Uganda imesimamisha mipango ya kujenga kituo cha umeme wa maji karibu na hifadhi ya Murchison Falls, huku waendeshaji wa sekta ya utalii wakisema kuwa mradi huo utaathiri maadhari ya eneo hilo.
Waziri wa Utalii Ephraim Kamuntu amesema baraza la Mawaziri limekubaliana kuwa mradi uliopendekezwa wa megawati wa 300 kwenye mto Nile ungeathiri mazingira na utalii baadaye.
Zaidi ya watalii 100,000 hutembelea mbuga hiyo kaskazini magharibi mwa Uganda kila mwaka.
Mapema mwaka huu Mamlaka ya Udhibiti wa Umeme ya Uganda ilitangaza kuwa kampuni ya Afrika Kusini, Bonang Power and Energy Pty (Ltd), ilikuwa imeomba leseni ya kujenga bwawa la umeme kwenye eneo la Uhuru.

No comments :
Post a Comment