dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, September 21, 2019

Kampeni ya 'fukua fukua' Tabora mjini yazaa matunda!

Serikali ya Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama Mkoani humo wameendesha Kampeni  maalumu ya kukabiliana na uhalifu iliyopewa jina 'fukua fukua' katika Manispaa ya Tabora huku baadhi ya watu ambao wanaodaiwa kutajwa kuwa ni wahalifu  baada ya zoezi la  upigaji wa  kura za siri na wakijitokeza kujisalimisha hadharani  kabla ya Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua za sheria .

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akisimamia kampeni kata ya isevya  ambayo inatajwa kuwa kinara  wa matukio ya uhalifu ikiwemo uuzaji wa dawa za kulevya  pamoja na ujambazi wa kutumia silaha ambayo matukio hayo  ya uhalifu ambayo kwa kiasi kikubwa yamekua yaki gharimu maisha ya watu na  mali zao.
"Mwananchi yoyote anae jisikia vibaya na hii oparesheni tunamuomba atupishe tutakapokuwa tumemaliza kupiga kura hapa  na  kama jina lako limesomwa hapa kwa uhalifu  inatakiwa ukalipoti kituo cha polisi  nausipo enda tutakusaka kama panya," Amesema Mwanri.

Katika kampeni hiyo mkuu wa wilaya ya Tabora Komanya Erick Kitwala amewaomba wananchi wa kata hiyo kutoa ushirikiano kwa kampeni hiyo  ili wahal ifu waweze kupatikana  isevya na mkoa wa Tabora kwa ujumla uweze kuwa shwari.

"Mtoe ushirikiano kwenye kampeni hii ya fukua fukua hatuko tayari kuona manispaa ya Tabora  manispaa ambayo inakuwa  watu wasishidwe  kuwekeza   kwa kuogopa ujambazi ,wizi, hawa majambazi ,vibaka,wauza madawa wavuta bangi sisi tunakaa nao na tunawaju’’Amesema Komanya.

Nae Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, ACP Barnabas Mwakalukwa amewasisitiza wananchi watakaoandika majina ya wahalifu hao waweze kuandika uhalifu wanaoufanya ili kuwabaini kiuharaka zaidi na si kumuandika mtu ili kumkomo.

Hata hivyo mara baada ya  wananchi kupiga kura za siri  na majina ya watu wanaodaiwa kuwa wahali nfu kusomwa hadharani  ambapo baadhi yao wameamua kujisalimisha wenyewe hadharani ili kuepuka mkono wa dola.

No comments :

Post a Comment