Uganda imesaini makubaliano na Urusi kuisaidia kujenga uwezo wake wa kutumia teknolojia ya nyuklia kwa matumizi ya kutengeneza nishati, dawa na matumizi mengine ya amani.
Hatua hii inafuatIa kusainiwa kwa makubaliano mnamo Mei mwaka jana baina ya serikali ya Rais Yoweri Museveni na shirika la kitaifa la nyuklia China CNNC, kulisaidia taifa hilo la Afrika Mashariki kuendeleza matumizi ya nishati ya nyuklia kwa madhumuni ya amani.
Katika ujumbe rasmi wa Wizara ya Nishati Uganda, makubalinao hayo na Urusi yalisainiwa hapo jana Jumatano huko Vienna kati ya Waziri Irene Muloni na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Nishati ya Atomiki ROSATOM, Nikolai Spasskiy.

No comments :
Post a Comment