dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, June 28, 2020

WANAOGOMBEA KITI CHA DR. SHEIN KUTOKA CCM KWA MWAKA 2020 MPAKA SASA NI HAWA HAPA!


1. Mbwana Bakari Juma
2. Ali Abeid Karume
3. Mbwana Yahya Mwinyi :
4. Omar Sheha Mussa
5. Hussein Ali Mwinyi
6. Shamsi Vuai Nahodha
7. Mohammed Jaffar Jumanne
8. Mohammed Hijja Mohammed
9. Issa Suleiman Nassor
10. Makame Mnyaa Mabarawa
11. Mwatum Mussa Sultan
12. Haji Rashid Pandu
13. Abdulhalim Mohammed Ali
14. Jecha Salum Jecha
15. Dk Khalid Salum Mohammed
16. Rashid Ali Juma
17. Khamis Mussa Omar
18. Mmanga Mjengo Mjawiri
19. Hamad Yussuf Masauni.
20. Mohammed Aboud.
21. Bakar Rashid Bakari
22. Hussein ibrahim makungu
23. Ayoub Mohammed Mahmoud
24. Hashim Salum Hashim
25. Fatma kombo Masoud
26. Hasna Attai Masoud
27. Maalim Iddi Hamad Iddi
28. Pereira Ame Silima
29. Shaame Simai Mcha

30. Mussa Aboud Jumbe
31.  Mgeni Hassan Juma


Ratiba ya Mchakato wa Kupata Wagombea wa CCM Urais JMT & Zanzibar


15 – 30/06/2020
Kuchukua na kurejesha fomu. Mwisho wakurudisha fomu ni tarehe 30/6/2020 Saa 10:00 jioni.

15 – 30/06/2020
Kutafuta wadhamini Mikoani. 
VIKAO VYA UCHUJAJI

01 – 02/07/2020
Kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar.

03/07/2020
Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili Zanzibar. 

04/07/2020
Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar: Kufikiria na kutoa Mapendekezo yake kwa Kamati Kuu kuhusu wanachama wanaoomba nafasi ya Rais wa Zanzibar.

09/07/2020
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa: Kufikiria na kutoa Mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa juu ya majina ya wanachama wasiozidi watatu wanaoomba kugombea kiti cha Rais wa Zanzibar.

10/07/2020
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa: Kuchagua jina moja la mwanachama atakayesimama kugombea Urais Zanzibar.  

11 - 12/07/2020
Mkutano Mkuu wa CCM Taifa: Kuthibitisha  jina la mwanachama atakayesimama katika Uchaguzi wa Rais wa Zanzibar.

MAMBO YA KUZINGATIWA NA KILA MGOMBEA 
  1. Kila mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni lazima apate wadhamini 250 katika Mikoa 12 angalau Mikoa 2 kati ya hiyo iwe ya Zanzibar.
  2. Kila mgombea wa Urais wa Zanzibar ni lazima apate wadhamini 250 katika Mikoa isiyopungua mitatu, kati ya hiyo angalau Mkoa mmoja kutoka Unguja na mmoja kutoka Pemba. 
  3. Wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa hawaruhusiwi kumdhamini mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  4. Wajumbe wote wa Halmashauri Kuu ya Taifa hawaruhusiwi kumdhamini mgombea Urais wa Zanzibar. 
  5. Mwanachama haruhusiwi kumdhamini mgombea zaidi ya mmoja. 
  6. Fomu ya udhamini ya wanachama ithibitishwe na Katibu wa CCM wa Wilaya kwa kupigwa muhuri wa chama wa Wilaya husika. 
  7. Wanachama watakaomdhamini mgombea, uanachama wao uthibitishwe na Katibu wa CCM wa Wilaya husika.
  8. Kila mgombea atalazimika kuzingatia maadili ya Chama Cha Mapinduzi, masharti ya uongozi, sifa za wagombea na utaratibu wa kuomba uongozi kama ilivyofafanuliwa katika Kanuni za Uteuzi wa wagombea uongozi katika vyombo vya Dola, Kanuni za Uchaguzi na Kanuni za Uongozi na Maadili.

No comments :

Post a Comment