dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 12, 2021

Afya: Fahamu homoni 4 zinazochochea furaha maishani!

 

Mental Healh: तुमचा मूड सतत जातो का? मग या 4 हार्मोन्सकडे लक्ष द्या

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Wengi wetu hatufikirii juu ya homoni katika maisha yetu ya kila siku. Tunajua kwamba kuna homoni katika miili yetu, mabadiliko ya homoni kwa wavulana na wasichana wanapobaleghe.

Wanawake wanasadikiwa kuwa na 'hormonal' angalau mara moja wakiwa na hedhi

Wengi wetu tunajua angalau jukumu la testosterone na estrojeni katika ukuaji wa binadamu.

Homoni huendesha kila kitu maishani mwetu - ndio maana wakati mwingine unajisikia vizuri, wakati mwingine unajisikia vibaya, wakati mwingine unakasirika, yote haya hutokana na mabadiliko ya homoni.

Homoni ni nini, zinatoka wapi?

Homono ("kichochezi", "msukumo") ni kemikali zinazotolewa na tezi za mwili na kusafiri kupitia mfumo wa mzunguko wa damu hadi ogani za mwili. Humo zinasababisha mabadiliko katika kazi ya ogani.

Mental Healh: मूड चांगला ठेवायचा आहे? मग या 4 हार्मोन्सकडे लक्ष द्या

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mwili wetu huwasiliana na yenyewe kupitia homoni. Tezi ya pituitari, tezi, tezi ya adrenalini, ovari na korodani zote ni sehemu ya shirika hili. Kwa ujumla kuna viungo vingi visivyojulikana.

Ushawahi kujiuliza jinsi akili na miili yetu hufanya kazi pamoja. Hiyo ndiyo sababu mojawapo iliyonifanya kuwa tabibu,alisema mtaalamu mmoja

Happy Hormones म्हणजे काय? त्यांची पातळी कशी वाढवता येते? त्यासाठी काय खावे, कोणता व्यायाम करावा?

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kazi za homoni inachangia karibu kila tabia katika maisha yetu, lakini huenda tusiwe na ufahamu wa kile kinachotokea.

Kwa mfano, unapozungumza na watu wako wa karibu, je, unahisi upendo na kuongezeka kwa hisia ya furaha?

Hali hiyo inachangiwa na homoni inayojulikana kama oxytocin. Inahimiza tabia zinazoimarisha uhusiano wa kifamilia.

Je, unajisikia kuwa na nguvu na kuridhika unapokimbia? Hali hiyo inachangiwa na homoni ya endomorphin. Wakati huo ufahamu wako wa maumivu hupungua na hisia za furaha huongezeka.

Masiha yangelikuwa vipi ikiwa tungefanya mambo yanayochangamsha homoni kimakusudi, badala ya kungoja homoni kutolewa kwa njia za kiasilia za maumbile tunapofanya mambo yanayotufanya tujisikie vizuri?

Na je hali ingelikuwa vipi iwapo ungechochea homoni hizo katika kazi yako, wakati wa tafrija na katika mahusiano ili kuwa na afya njema? Bila shaka tungelikuwa na uwezo wa mkubwa wa kuishi kwa furaha nyakati zote.

Wapenzi

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Zifiuatazo ni homoni 4 unazotakiwa kuimarisha ili kuwa na furaha:

Oxytocin

Oxytocin ni homoni muhimu ya 'upendo' ambayo itaboresha uhusiano wako. Homoni hii hutolewa unapojisikia salama, unapojumuika na watu wengine au kuwa karibu na watu katika imani yako.

Madhumuni ya homoni hii ni kuimarisha uhusiano kati ya wanadamu, ili wazazi waweze kuwa karibu na watoto wao, kudumisha muundo wa familia na kusaidia wanandoa kupata ukaribu zaidi.

Mental Healh: तुमचा मूड सतत जातो का? मग या 4 हार्मोन्सकडे लक्ष द्या

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Ili kuchochea homoni hizi kiasili:

  • Cheza wanya wanaofugwa nyumbani kama vile sungura au paka
  • Watendee hisani marafiki au familia kwa upendo
  • Unapaswa kuthaminiwa
  • Mazungumzo ya ana kwa ana na umpendaye
  • Jikande au upate mtu akukande
  • Andaa chakula na ule na uwependao

Serotonin

Ni homoni inayofanya kazi nyingi sana mwili , homoni hii hujulikana kama homoni ya utulivu kwa sababu homoni hii huweza kuchochea mtu kuwa na utulivu.

Waganda wakifanya mazoezi ya mwili
Maelezo ya picha,

Wataalamu wanashauri kuwa mazoezi ya misuli ni muhimu katika kuimarisha mifupa ya mwili hasa unapoongeza shinikizo kwa mifupa yako kwa njia ya mazoezi

Hufanya kazi kama homoni na kama mjumbe(nyurotransimita) wa taarifa

Husafirisha ujumbe kati ya seli moja ya neva na nyingine

Serotonin huzalishwa katika utumbo, ubongo, mfumo wa neva na chembechembe sahani za damu.

Homoni hii imehusishwa na udhibiti wa hisia, usingizi wa usawa, furaha na wasiwasi.

Ili kuchochea homoni hizi kwa kiasili:

  • Simama kwenye jua kwa muda kidogo
  • Kimbia, ogelea au endesha baisikeli
  • Chukua muda wako kutafakari mambo
  • Tembea katika mandhari ya kupendeza

Dopamine

Hii ni homoni kuwajibika kwa hali ya kisaikolojia ya hisia ya mtu. Inasaidia utendaji kazi wa moyo na ubongo, husaidia kudhibiti uzito na ni wajibu wa utendaji.

Inahamasisha mwili wetu kupata zaidi (motisha ya kupata zaidi katika suala la chakula na mafanikio ni muhimu.

Ukosefu wa homoni hii katika mwili wa binadamu husababisha hali ya mara kwa mara ya huzuni, na mkusanyiko wa uzito kupita kiasi.

Ili kuchochea homoni hizi kwa kiasili:-

  • Kula chakula unachopenda
  • Sherehekea ushindi mdogo katika maisha ya kila siku
  • Jitunze
  • Sikiliza muziki mzuri
  • Unapaswa kukamilisha kazi au mradi ambao umeanzisha

Endorphins

Homoni ya endorphin ni dawa ya asili ya kutuliza maumivu.Inasaidia kutibu maumivu, kupunguza msongo wa mawazo, na kuongeza furaha.

Unapokula chakula homoni ya endorphins' hutolewa, hivyo huufanya ubongo wako ujisikie furaha. Endorphins ni homoni maalum ambayo ikitolewa humfanya mtu kujisikia raha.

Oxytocin, Serotonin, Dopamine, Endorphin, ऑक्सिटोसीन, सेराटोनिन, डोपामाइन, एन्डॉर्फिन. Mental Health, मानसिक आरोग्य Happy Hormones BBC Marathi, बीबीसी मराठी

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Ili kuchochea homoni hizi kiasili:

  • Fanya mazoezi
  • Cheza na marafiki au tazama/ sikiliza vipindi vya vichekesho
  • Kula chokoleti
  • Maono ya kisanii yanapaswa kudumishwa
  • Jaribu kutumia mafuta kama vile lavender, machungwa, au ubani, nk.
  • Na bila shaka ngono.

Kwa hivyo, kufanya ubongo na mwili wako kujisikia katika hali nzuri, ni vyema kuzingatia baadhi ya mienendo kila siku ili kuchochea homoni zinazohitajika.


No comments :

Post a Comment