Sherehe hizo zilihudhuriwa na Wa-Tanzania kadhaa kutoka sehemu mbali mbali za Canada na pia zilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Canada H.E. Dr. Mpoki Ulisubisya.
Sherehe hizo za Uhuru zilifanyika nje kidogo ya jiji la Toronto kwenye hoteli maarufu ijulikanayo kama Hilton Garden Inn, Toronto Airport, kwenye Drive ya Caroga #3311, Mississauga, Ontario.
Habari muhimu iliyosambazwa katika sherehe hizo ni kuwa Balozi atakuwa na mkutano wa zoom tarehe 11 December saa 11 za jioni (Eastern) na topic itakuwa: TANZANIAN DIASPORA IN CANADA REFLECTING ON THE PAST 60 YEARS pamoja na kujibu masuala ya Wana-Diaspora.
Anaepewa mkono ni H.E. Dr. Mpoki Ulisubisya - High Commissioner wa Tanzania nchini Canada, kulia yake ni Board Member wa Jumuiya ya ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association) Nd. Hemed Zahor.
Support us by considering joining our Patreon scheme at:
BECOME A PATRON TODAY!
No comments :
Post a Comment