dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 8, 2021

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI WAANZA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA UHURU WA TANZANIA BARA!


Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani umeanza maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa kuadhimisha Siku ya “Wekeza Tanzania” jijini Dallas, Texas na kukutana na Diaspora wa Tanzania jijini Houston, Texas.
Mheshimiwa Dkt. Elsie Sia Kanza, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani akiwa na wadau mbalimbali wa maendeleo wakijiandaa na Mkutano kuhusu masuala ya uwekezaji kati ya Tanzania na Marekani, katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Miaka 60 ya Uhusiano na Ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani.
Mheshimiwa Balozi Dkt. Kanza akiwa anasisitiza jambo wakati wa Mkutano huo.
Mkutano ukiwa unaendelea kwa kushirikisha Washiriki kutoka Tanzania.
Mheshimiwa Balozi Dkt. Elsie Sia Kanza akiwa na Meja wa Jiji la Dallas, Mstahiki Meya Eric Johnson baada ya mazungumzo yao kuhusu Wafanyabiashara wa Dallas kuwekeza nchini Tanzania. Mkutano huu ulikuwa ni sehemu ya Siku ya “Wekeza Tanzania” katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Miaka 60 ya Uhusiano na Ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani.
Kikao baina ya Mheshimiwa Balozi Dkt. Elsie Kanza na Meya Eric Johson kikiendelea.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi
Mheshimiwa Balozi Kanza akihutubia Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Marekani, Diaspora za Tanzania, Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Nchi za Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakati wa Hafla iliyohusisha wafanyabiashara hao iliyoandaliwa na Ubalozi katika kuadhimisha siku ya “Wekeza Tanzania”, katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara na Miaka 60 ya Uhusiano na Ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani.
Baadhi ya washiriki wa Hafla hiyo wakisikiliza hotuba kuu ya ufunguzi kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Balozi Kanza akizungumza na baadhi ya washiriki wa Hafla hiyo.
Bi. Jessica Gordon, Mkurugenzi wa Huduma za Biashara, Ofisi ya Dallas-Fort Worth kutoka Wizara ya Biashara ya Marekani akizungumza kwenye Hafla hiyo.
Baadhi ya Washiriki wa Hafla hiyo.
Katika mwendelezo wa maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Mheshimiwa Balozi Elsie Kanza alifanya Mkutano na Diaspora wa Tanzania jijini Houston, Texas. Mkutano ulijadili masuala mbalimbali muhimu kwa maendeleo ya Taifa, ambapo Mhe. Balozi alipokea changamoto mbalimbali na kuahidi kuzifanyia kazi. Aidha, Mhe. Balozi aliahidi Ubalozi kufanya kazi kwa ukaribu na Diaspora kwa maendeleo ya Tanzania.
Mheshimiwa Balozi na Afisa wa Ubalozi, Bw. Malik S. Hassan wakiwa kwenye Mkutano huo na Diaspora.

No comments :

Post a Comment