dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 17, 2013

Dk Shein aonya migogoro ya ardhi

NA MWINYI SADALLAH

16th March 2013


Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein
Viongozi wenye dhamana wa ardhi Zanzibar wametakiwa kumaliza migogoro ya ardhi katika ukanda wa utalii Mkoa wa Kaskazini Unguja haraka kabla ya serikali kuu haijachukua hatua.

Agizo hilo limetolewa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, baada ya mkoa huo pamoja na Mkoa wa Kusini kukabiliwa na migogoro mikubwa ya ardhi tangu kuimarika kwa sekta ya utalii katika ukanda huo.

Dk Shein alitoa agizo hilo katika kikao cha majumuisho baada ya kukamilisha ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo kilichofanyika  Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja jana.

Alisema wakati umefika wa kumaliza migogoro ya ardhi Zanzibar na kuwataka viongozi wa mkoa, Wizara Ardhi, Makaazi Maji na Nishati na taasisi nyingine kuchukua hatua za haraka kumaliza migogoro hiyo.

Dk Shein alisema viongozi wa serikali yake  wanajukumu la kuhakikisha ufumbuzi wa migogoro ya ardhi inatapatikana na kuepuka kuanzisha mipya katika ukanda huo.
Hata hivyo alisema hakuna njia ya kumaliza matatizo kwa njia ya mkato badala yake viongozi kwa kushirikiana na wananchi wana nafasi kubwa ya kumaliza migogoro katika maeneo yao.

Alisema serikali ya awamu ya saba haitokubali kuona migogoro mipya ya ardhi inaendelea kujitokeza na kuwataka viongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kuepusha migogoro mipya kujitokeza katika ukanda wa mashariki wa Zanzibar.

Kuhusu udhalilishaji wanawake na watoto, Dk Shein, alisema serikali itaendelea kupambana na vitendo hivyo ikiwemo ubakaji pamoja na takwimu kuonyesha kupungua katika mkoa huo.

Alisema matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji yamepungua kutoka kesi 88 mwaka 2011 hadi 63 mwaka jana.

 “Pamoja na mafanikio kwa kushirikiana  na wananchi uongozi wa Mkoa hauna budi kuendelea kukabiliana na vitendo vya uzalilishaji wanawake na watoto Zanzibar,”alisistiza  Dk shein.

Hata hivyo Takwimu zinaonyesha mwaka  2010 hadi 2011 jumla ya kesi za udhalilishaji ikiwemo matukio ya ubakaji 127 zilifunguliwa, lakini kati ya kesi 66 zilizosikilizwa na kutolewa hukumu washitakiwa watatu tu ndiyo walipatikana na hatia kwa Unguja na Pemba.

Dk Shein katika ziara yake ya mikoa mitatu ya Unguja alikagua miradi ya maendeleo katika sekta ya Maji, Elimu, Mazingira, ufugaji wa samaki, nyumba za makazi pamoja na harakati za wajasiriamali visiwani Zanzibar.


CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment