Salma Said,
ZANZIBAR: Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeahidi kuanzisha Taasisi ya kusimamia biashara ya mafuta, umeme na maji (ZURA) ili kuondosha ubadhirifu usitokee katika vituo vya kuuzia mafuta (petrol station).
Naibu Waziri wa Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati , Mhe. Haji Mwidini Makame ameyasema hayo wakati akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo (CCM) Nassor Salim Ali aliyetaka kujua ni kwa sababu gani baadhi ya wafanyabiashara wenye kutoa huduma za kuuza mafuta hufanya mafuta hayo kuadimika na baadae nishati hiyo huuzwa kwa magendo.
Naibu Waziri huyo alisema wizara yake anayoifanyika kazi hivi sasa imo katika mchakato wa kuanzisha taasisi inayojitegemea ya kusimamia biashara hiyo ya nishati kwa nia ya kuondoa ubadhilifu unaofanywa na watu ambao hawana nia njema katika kutoa huduma kwa wananchi.
Akijibu suali hilo katika kikao cha kumi na moja cha baraza la nane la Wawakilishi Mhe. Makame aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba chanzo cha tatizo hilo kinatokana na kuchelewa kuingizwa mafuta ya petrol kwa baadhi ya makampuni yanayofanya biashara hiyo lakini sheria itakayopitishwa itaweka chombo maalum cha kusimamia matatizo hayo.
Alisema lengo la Serikali ni kuunda chombo hicho ambacho kitakachokuwa na uwezo wa kisheria wa kusimamia masuala yote hayo yanayohusiana na mambo hayo na hivyo kwa kiasi kikubwa tatizo la usumbufu wa wananchi utaondoka.
Akichangia mswada wa sheria ya udhibiti wa huduma ya maji na nishati, Mwakilishi wa Magomeni (CCM) Salmin Awadh Salmin huko katika ukumbi wa baraza la Wawakilishi huko Chukani nje kidogo na mji wa Zanzibar alisema kuanzishwa kwa sheria hiyo mamlaka ya udhibiti wa huduma ya maji na nishati Zanzibar kutadhibiti mambo mengi ikiwemo kupandishwa bei mara kwa mara kwa nishati hio .
Alisema bidhaa hiyo ya mafuta imekuwa ikileta mizozo na mkanganyiko kwa wenye vyombo kwa madai kuchanganywa kwa mafuta na maji kuchanganywa kwa mafuta ya dizeli na ya taa na kusababisha uharibifu mkubwa kwa gari za watu.
Mwakilishi huyo alisema kuwa kumekuwa na tatizo la muda mrefu juu ya namna ya kudhibiti mafuta lakini hata upandaji wake huwa unalazimisha mambo mengi kupanda kwa bei jambo aambalo linaonesha hakuna mambo madhubuti ambayo yanadhibiti mafuta.
Awadh alisema kuazishwa kwa sheria hiyo kutasaidia kusimamia huduma inayotolewa ili iwe yenye ubora kulingana na viwango vilivyowekwa na sheria hiyo na kuepuka kupatikana mafuta yasiyo na kiwanago na kero za matatizo hayo itaondoka kwa kiasi kikubwa.
Nae Mwakilishi wa Jimbo la Chonga (CUF) Abdalla Juma Abdallah alisema mambo mengi ambayo yanapatikana katika kupandishwa mafuta ovyo na kuchanganywa maji na mafuta nib jambo ambalo halipendezi na linaathiri kwa kiasi kikubwa gari za watu na kuiomba serikali kusimamia jambo hilo.
Alisema wafanyabiashara wengi hivi sasa wamekuwa wakiuza vitu visivvo na viwango na hivyo kusababisha kukosekana ubora wa bidhaa ambapo alisema ni muhimu kuwekwa sheria kali za viwango vya bei na ubora ili kuwasaidia wananchi.
“Matumaini yangu chombo hicho kitangalia sana ubora unaotakiwa kwani sisi wajumbe wa baraza la wawakilishi wengi wetu hatuna taluma za sheria nilikuwa nataka hawa wanasheria kuandika kitu kizuri wanasheria wetu wangekuwa makini zaidi kabla hawajatuletea sisi hapa.” alisema Abdallah.
Hata hivo alisema vyanzo vya maji sasa vimeharibika sehemu nyingi zilizokuwa zikipatikana maji zilikuwa na miti sasa zimeharibiwa kwa kukatwa miti hiyo ambayo ikileta ubaridi na sasa maji mengi yyakauka kwa upepo na kupelekea vanzo hivo kuharibika
“Tunaomba wizara kuboresha sehemu zile ili kuona nishati ya maji inarudi kwenye hadhi yake tukilinyamazia hili tutaona siku moja rasilimali ra maji imepoteza hadhi yake “alisema mwakilishi huo .
Alisema Wananchi ikiwa hali zao nidhaifu kiuchumi lakini ZAWA ni dhaifu kutoa huduma kutokana na mapungufu ya maji kwa siku moja kwa ajili ya kukizi mahitaji akalipa zaidi ya shilingi elfu tano kununua maji ya siku moja .
“Ikiwa zawa imeweka kiwango cha shilingi elfu 2500 hicho ni kiwango kizuri ZAWA nayo haiwezi kufikisha maji bila ya michango sasa tufanye vipi tufikishe fedha mwanzo au tupate maji mwanzo asa ombi langu kwa wananchi walipie maji ili tufikie lengo” alisema Mwakilishi huyo.
No comments :
Post a Comment