dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, June 24, 2013

JUMUIYA YA ZIRPP YAWATAKA WAZANZIBAR KUIENZI SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA

Na Hamed Mazroui

Jumua ya Zanzibar Insitute for resarch and public policy imewapa nafasi wawakilishi kutoka sehemu mbali mbali za Zanzibar kutoa maoni yao kuhusu faida na changamoto za serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar .
Katika mjadala huo ambao mtoa mada alikuwa ni Mzee Enzi Aboud, umfanyiaka katika ukumbi wa jumua hio uliopo Vuga mjini Unguja.
Wakati akitoa mada Mzee Enzi amesema kuwa Zanzibar ni nchi ya kidmocrasia,wananchi wa Zanzibar ndio wenye mamlaka ya nchi yao,pamoja na hayo Mze Enzi alisma mengi sana,miongoni mwa aliyosema ni kuwepo kwa faida na changamoto zinazoikabili SUK.
Chama cha wananchi CUF kupitia mjumbe wake Muhammed Nnur kimesema kuwa ipo haja ya kuangaliwa upya katiba ya Zanzibar kwani katiba iliopo hivi sasa inaifanya kuwa sera zinazoongoza serikali kuwa ni sera za chama tawala CCM jambo ambalo inaifanya jamii kuona chama cha wananchi CUF hakifanyi kazi yoyote ndani ya serikali.
Akiendelea kutoa baadhi ya changamoto zinazoikabili SUK hapa Zanzibar nikutokuwepo kwa uwazi ndani ya tume ya uchaguzi licha ya kuwa kila mara inalalamikiwa na wananchi lakini bado imekuwa ikifanya makosa yale yale kila ifikapo kipindi cha uchaguzi mkuu hapa Zanzibar ‘’nadhani tunakumbuka hata katika uchaguzi mkuu uliopita licha ya Maalim Seif kuyakubali matokeo lakini alionesha wazi kutokuridhishwa kwake na tume ya uchaguzi”alisema Muhammed nnur.
Amefahamisha kuwa wakati wa kura ya maoni ya kuleta suk asilimia kubwa ya wazanzibar walipiga kura na kuikubali serikali hii,kuwpo kwa asilimia kubwa kunaonesha wazi kuwa wazanzibari wnyewe ndio wameitaka serikali hii.
Aidha nae muwakilishi katika mdahalo huo kutoka chama cha mapinduzi CCM Bwana Ali Mwinyi Msuko amesema kuwa chambuko kabisa cha serikali ya umoja wa kitaifa limezaliwa ndani ya CCM,pale mwenyekiti wa chama hicho Raisi kikwete aliposema hadharani kuwa haridhishwi kabisa na mpasuko wa kisiasa ulipo Zanzibar ndipo ikaundwa tume maalumu ya kushughulikia jambo hilo na tayari walishafikia makubaliano kuwa wananchi wenyewe ndio waulizwe kupitia kura ya maoni lakini cha kushangaza chama cha CUF kikakwepa azimio hilo la Butiama.
Pamoja na kutokea hayo yote wao kama chama cha CCM hawakufurahishwa na hali ya kisiasa iliokuwepo Zanzibar ya mtafaruk kila ifikapo uchaguzi mkuu wakati waathirika ni wazanzibar wenywe na ndio maana Rais karume alipozungumza na Maalim Seif juu ya jambo hili wao hawakulipinga na walilikubali moja kwa moja kutokana ni jambo muhimu sana kuwepo hapa Zanzibar.
Akizungumzia kuhusu muundo wa serikali ya umoja wa kitaifa kuwa umegawa madaraka kwa nafasi za juu tu yaani mawaziri na makamo wa kwanza amesema kuwa kuna makosa yamefanyika na ilistahiki hadi nafasi nyengine zishirikishe watu kutoka sehemu nyengine na isiwe kama ilivo hivi sasa.
‘’Naomba wazanzibar tuwe wastahamilivu juu ya hili kidogo kidogo ndio mwendo itafika wakati hata hizo nafasi za chini kabisa za masheha zitakuwa za uwiano mambo huenda kwa hatuwa tunachopaswa kwa sasa nikushukuru kufikia alau hatuwa hii iliopo”alisema Ali Mwinyi.
Sambamba na hayo amebainisha kuwa katika nchi yetu ya Zanzibar kuna tatizo kubwa la kiuchumi jambo ambalo limeifanya nchi yetu kutokupiga hatuwa mbele kimaendeleo lakini “haya yote yanasababishwa na uwepo wa wingi wa viongozi serikalini pamoja na kupewa mishahara mikubwa kwa wakurugenzi na mawaziri ‘’utakuta wizara moja ina wakurugenzi zaidi ya watatu na wanalipwa mishahara mikubwa sana wakati wananchi wa chini wanalalamika kipato chao nikidogo mno”alieleza Ali Mwinyi.
Nae mwanasheria maarufu hapa Zanzibar Bwana Awadhi amesema kuwa kuwepo kwa amani ndani ya nchi ni jukumu la kila serikali yoyote hile ulimwnguni isipokuwa kukiwa na serikali ya umoja wa kitaifa ndio inaongezewa mzigo mkubwa zaidi wa kuhakikisha muda wote amani inatawala.
Akibainisha baadhi ya changamoto zinzoikabili serikali ya umoja wa kitaia Zanzibar ni kuwa SUK hapa kwetu bado ni changa hivo baadhi ya changamoto zinazoikabili ni kutokana na uchanga wake.
Kwa upande wao baadhi ya wachangiaji katika mdahalo huo wamesema kuwa kuwepo kwa changa moto katika suk inatokana na baadhi ya watu kuwa na utashi wao binafsi wa vyama vyao vya kisiasa.
Wakizungumzia kuhusu faida nyengine za SUK ni kuwaona wawakilishi ndani ya baraza la wawakilishi kwa umoja wao wakiibana vikali serikali yao bila ya kujali itikadi ya vyama vyao vya kisiasa.
Jumua ya Zanzibar Insitute for resarch and public policy imekuwa ikihusika na mambo mbali mbali ya kijamii hapa Zanzibar sambamba na kutoa ushauri wa mambo mbali mbali.

Chanzo: Mzalendo.net

No comments :

Post a Comment