Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya Maendeleo ya Elimu (Tedro) iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jacob Kateri, alisema katika uzinduzi wa ripoti hiyo jana Lowasa alipata asilimia 26 baada ya watu 1,200 katika mikoa sita ya Tanzania Bara kuhojiwa.
Wanasiasa wengine waliotajwa katika ripoti hiyo kwamba, wana uwezo wa kusimamia sekta hizo na alama zao kwenye mabano ni Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (23%), Dk. Willibroad Slaa (22%), Profesa Ibrahim Lipumba (7%), Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (6%) na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (5%).Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya (4%), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe (3%) na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirikia, Stephen Wasira (1.8%).
Alisema lengo la utafiti huo ni kuangalia jinsi sekta ya elimu inavyoweza kuinuka kwa kuzihusisha na sekta nyingine za afya na maji.
Alitaja mikoa na wilaya, ambako utafiti huo ulifanyika kuwa ni Dar es Salaam (Temeke), Pwani (Wilaya Kibaha Mjini), Dodoma (Bahi na Chamwino), Manyara (Mbulu na Babati Mjini), Ruvuma (Songea Mjini, Namtumbo) na Tabora (Nzega na Tabora Mjini).
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment