dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, September 9, 2015

Afya ya Mabere Marando yaimarika


Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Mashariki ambaye pia ni mwanasheria, Mabere Marando .

By Herieth Makwetta, Mwananchi
Dar es Salaam. Afya ya Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Mashariki ambaye pia ni mwanasheria Mabere Marando, imeanza kuimarika na leo alifanyiwa vipimo kadhaa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikolazwa.
Marando alifikishwa hospitalini hapo Jumapili jioni akiwa hajitambui baada ya kuugua ghafla akiwa nyumbani kwake na kulazwa katika jengo la tiba la magonjwa ya upasuaji wa moyo, katika wodi maalum za kulipia FF4 chumba namba 2.
Akizungumza na Mwananchi leo Ofisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili John Stephen, alisema hali ya Marando inazidi kuimarika huku akiendelea kupatiwa matibabu na madaktari bingwa.
“Leo amefanyiwa vipimo kadhaa na hali yake sasa inaridhisha, familia bado haipo radhi kuzungumza chochote na isingependa kuonana na vyombo vya habari kwa sasa na iwapo atapata nafuu ataweza kuzungumzia nini zaidi kinamsumbua,” alisema Stephen.
Mmoja wa wauguzi wa hospitali hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake, alisema Marando alifikishwa hospitalini hapo akiwa na hali isiyoridhisha.
“Hana tatizo la moyo bali anaonekana kuzidiwa baada ya kufanya kazi kupita kiasi. Si mgonjwa sana ila anasumbuliwa kiasi anaonekana amefanya kazi kwa muda mrefu na hivyo kukosa wasaa wa kupumzika, madaktari wamempatia matibabu maalum kwa ajili ya kuirudisha afya yake katika hali ya kawaida.”

No comments :

Post a Comment