dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, September 8, 2015

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Pemba Ndg Jabu Khamis Mbwana Afariki Dunia Usiku wa kuamkia leo.


Mhe Jabu Khamis Mbwana alipoapishwa kuwa Mkuu wa Wilaya na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Dr A|li Mohamed Shein. 

Innaa lillaahi wainnaa ilayhi Raaji'un

Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Nd. Jabu Khamis Mbwana amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Kijiji kwake Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Marehemu Jabu alikuwa akisumbuliwa na homa kwa takriban wiki moja sasa na maziko yatafanyika huko Kiuyu saa nne za asubuhi leo hii.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Micheweni akiwa na fani ya Uandishi wa Habari na kufikia hatua ya Kuwa Afisa wa Habari wa Wilaya katika miaka ya 80 aliwahi kuwa Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Micheweni katika miaka ya mwishoni mwa 80.

Baadaye aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Wilaya ya Mkoani na kurejea Tena Wilaya ya Micheweni nafasi ambayo aliendelea nayo hadi muda huu mauti yalipomuhitaji.

Taarifa kamili ya wasifu wa Marehemu Jabu Khamis Mbwana zitapatikana baadaye.

Mwenyezi Muungu ampe safari njema Marehemu Jabu Khamis Mbwana. Amin.


Innaa lillaahi wainnaa ilayhi Raaji'un

No comments :

Post a Comment