Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Wa Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu Jaji Agustino Ramadhani wakizindua kitabu cha taarifa za msingi kuhusu mahakama hiyo kwenye Ukumbi wa Kibo kwenye majengo ya Mahakama hiyo mjini Arusha leo Septemba 10, 2015. Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuagana na viongozi na wafanyakazi wa mahakama hiyo, awali Rais Kikwete, alitunukiwa tuzo ya uongozi bora Ikulu jijini Dar es Salaam leo Septemba 10, 2015. Tuzo hiyo aliyotunukiwa nchini Afrika Kusini hivi karibuni, na kupokelewa kwa niaba yake na Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Asha Rose Migiro, ilikabidhiwa kwake katika hafla iliuyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Mahakama ya aFrika ya Haki za binadamu mjini Arusha wakati Rais alipotoa hotuba ya kuwaaga.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wafanyakazi na viongozi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu mjini Arusha leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Rais wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu iliyopo mjini Arsuha huku Rais wa Mahakama hiyo Jaji Agustino Ramadhani kulia akishuhudia
Rais Dkt,Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri mkuu Mizengo Pinda naRais Wa Mahakma ya Afrika Jaji Agustino Ramadhani muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili mjini Arsuha ambapo aliagana na Viongozi na wafanyakazi wa Mahakama ya Afrika leo. (Picha zote na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Mahakama ya aFrika ya Haki za binadamu mjini Arusha wakati Rais alipotoa hotuba ya kuwaaga.
Rais akitoa hotuba yake
No comments :
Post a Comment