dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, September 8, 2015

Lowassa: Kwanini kura hazitaibiwa.

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi Oktoba 25 ili wampe ushindi wa kishindo kwani anaamini kwamba hakuna kura itakayoibwa.
 
Lowassa anayewakilisha pia muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya NCCR-Mageuzi, NLD na Chama cha Wananchi (CUF), amesema ana imani kubwa kwamba katika uchaguzi mkuu mwaka huu, hakutakuwa na hila zozote za kuiba kura kwa maslahi ya chama tawala na kwamba wananchi wanapaswa kujitokeza kwa wingi na kumpa ushindi usiokuwa na shaka yeye na wagombea wenzake wote wanaowakilisha Ukawa.
 
Lowassa alisema hayo jana wakati akizungumza mbele ya umati wa wananchi waliofurika katika mkutano wa kampeni wa Chadema uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Bunju, Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam.
 
Alisema yeye na wenzake wanaounda Ukawa wamejipanga kuhakikisha kuwa hakuna kura inayoibwa.  
 
"Ninachowaomba ni kujitokeza kwa wingi na kutupigia kura kwa nia ya kuleta mabadiliko ya kweli... hakuna kura itakayobiwa," alisema Lowassa na kushangiliwa na umati uliofika kwenye mkutano huo jana.
 
AJIRA, FOLENI DAR, MAJI
Katika mkutano wake huo, Lowassa alirudia kauli yake kuhusiana na namna anavyoumizwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana na hivyo, akasema mara tu atakapoingia madarakani, miongoni mwa maeneo ambayo serikali yake itayafanyia kazi haraka ni juu ya namna ya kuhakikisha kuwa tatizo hilo linafanyiwa kazi.Akieleza zaidi, Lowassa alisema njia mojawapo kubwa ya kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira ni kuzalisha ajira mpya, hasa kwa kuhakikisha kuwa viwanda vingi vinajengwa ili mwishowe viongeze wigo wa ajira kwa Watanzania.
 
Kadhalika, Lowassa alisema anaguswa na kero ya msongamano wa magari kwenye maeneo ya miji kama Dar es Salaam na hivyo akichaguliwa atahakikisha serikali inamaliza tatizo hilo kwa kuimarisha miundombinu ya barabara, pamoja na kuzipanua zilizopo ili kukidhi mahitaji.
 
Kuhusiana na tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama, Lowassa alisema hakuna njia nyingine ya kuondoa tatizo hilo isipokuwa ni kwa kuhakikisha kwamba serikali inatumia rasilimali zilizopo kuwezesha upatikanaji wa huduma muhimu kwa maisha ya viumbe hai.
 
Alisema ana uzoefu mkubwa katika masuala ya maji kwani alishaongoza wizara inayoshughulikia maji na hivyo atatumia ujuzi na maarifa yake yote kumaliza tatizo hilo.
 
MICHANGO YA SHULE MARUFUKU 
Katika hatua nyingine, Lowassa alirudia kauli yake ya kuahidi elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu.
Alisema ili kufanikisha jambo hilo kwa vitendo, atakapochaguliwa na kuingia Ikulu atapiga marufuku michango yote ya elimu ili kuhakikisha elimu inakuwa bure na hivyo kuwapa fursa Watanzania wote kuipata bila kujali hali zao kiuchumi.
 
Alisema jambo hilo linawezekana na wala siyo la kufikirika kwani taifa lina rasilimali nyingi ambazo mapato yake yatatumiwa vizuri kuwezesha upatikanaji wa elimu bure kwa kila mmoja.
 
"Nitafanya kazi kwa spidi 120... jitokezeni na kupiga kura ili tulete mabadiliko ya kweli," alisema Lowassa na kuibua shangwe kubwa.
 
SUMAYE, MBOWE WANENA 
Awali, kabla ya Lowassa kuhutubia kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Bunju na pia kwenye mkutano mwingine alioufanya Mbezi Luis jirani na Stendi ya Mabasi katika Jimbo la Kibamba, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye alisema huu ni wakati mzuri zaidi kwa Watanzania kufanya mabadiliko ya kiuongozi kwa kuking'oa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuipa nafasi Ukawa. 
 
Alisema CCM ya sasa haiwezi tena kuleta mabadiliko yatakayowasaidia Watanzania na kwamba hata mgombea urais wao, Dk. John Magufuli, hatakuwa na jipya kwao na hivyo wasifanye makosa siku ya kupiga kura na badala yake wahakikishe wanampa kura nyingi za ndiyo Lowassa na wagombea wengine wa Ukawa.
 
Kadhalika, Sumaye alijibu mapigo kuhusiana na tuhuma wanazoibuka dhidi ya Lowassa hasa kuhusiana na kashfa ya mitambo ya kufua umeme ya Richmond kwa kuhoji kuwa ni kwa nini Magufuli na timu yake hawaelezi namna watakavyoshughulikia wahusika wa kashfa kama za uchotwaji wa fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow, utoroshaji wa twiga hai na pia ujangili wa meno ya tembo.
 
"Escrow Lowassa hakuwapo... Magufuli aseme hilo atalishughulikia vipi?  
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, aliwataka Watanzania kujiandaa kupokea mabadiliko kwani CCM haiwezi tena kuongoza nchi.
 
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ubungo ambaye sasa anagombea Jimbo la Kibamba, John Mnyika, alisema ni wakati sasa kwa wananchi wote kuungana katika kumpa ushindi Lowassa na wagombea wote wa Ukawa ili wailetee nchi maendeleo. Aidha, alimtaka Lowassa kuwaondolea kero ya maji wananchi wa Jimbo la Kibamba akiingia madarakani.

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment