dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, September 9, 2015

Magufuli: Serikali ya awamu ya tano itakuwa ya viwanda


Akiwahutubia wananchi leo katika Uwanja wa Tangamano mjini Tanga, Dk Magufuli amesema kuwa akichaguliwa kuwa rais atajenga viwanda vipya na kufufua vile ambavyo vimekufa ili wananchi wapate ajira na kuacha kuhangaika.
By Emmanuel Mtengwa, Mwananchi Digital
Tanga. Mgombea wa urais kupitia CCM, Dk John Magufuli amesema iwapo atapewa ridhaa ya kuwa rais atahakikishwa Tanga inakuwa mji wa viwanda.
Akiwahutubia wananchi leo katika Uwanja wa Tangamano mjini Tanga, Dk Magufuli amesema kuwa akichaguliwa kuwa rais atajenga viwanda vipya na kufufua vile ambavyo vimekufa ili wananchi wapate ajira na kuacha kuhangaika.
Amesema kuwa vipo viwanda vingi ambavyo vilijengwa zamani na sasa vimetelekezwa na vimebaki kama magofu hivyo serikali ijayo itavifufua.
“Serikali ya Magufuli ya awamu ya tano itakuwa serikali ya viwanda, tunataka tujenge viwanda vipya lakini pia tufufue vilivyokuwepo’’amesema Magufuli.
Akiendeleza kutoa hutuba yake ya kuomba kura huku akikatishwa na sauti za wananchi za kushangilia, Dk Magufuli ameeleza kuwa anataka serikali ya awamu ya tano itengeneze asilimia 40 ya ajira zitakazotokana na sekta ya viwanda.
Ameeleza kuwa serikali yake itajikita kujenga viwanda vya samaki katika mwambao mwa bahari ili nchi iweze kupata fedha na vijana wapate ajira.
’Nitajenga viwanda vikubwa vya samaki ili watu wa Tanga mpate ajira na watanzania kwa ujumla’’ alisisitiza Dk Magufuli.
Pia Dk Magufuli amewahakikishia wananchi wa Tanga kuwa atahakikisha mashamba ya mikonge yanaendelezwa na wale watakaoshindwa kuyaendeleza watanyanganywa.
‘’Najua wananchi wa Tanga wanashindwa kupata mashamba ya kulima, hivyo nitawaambia wawekezaji waendeleze mashamba yao na wasipoyaendeleza sitaona aibu kuwanyanganya na kuwapa wananchi wa Tanga bure’’ alidokeza Magufuli na kushangiliwa na wananchi.
Amewataka wananchi wamuombee ili pale atakapochaguliwa kuingia Ikulu asiwe na kiburi na aweze kuwakumbuka wananchi wa hali ya chini na kutekeleza ahadi zake.

No comments :

Post a Comment