dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, September 8, 2015

MAMBO HALISI : Tujisahihishe kwa hili, tuendako kubaya

  • Ninapenda kusema nieleweke tangu mwanzo kuwa binafsi siandiki mambo haya kwa kujifurahisha, kulalamika au nikiwa na mtazamo wa kuunga mkono kambi yoyote, kati ya mbili kubwa ambazo zimejiainisha kuwa na upinzani kwa sasa.
Ni imani yangu kwamba safari yetu bado ni salama licha ya mawimbi na misukosuko michache ambayo imeanza kujitokeza.
Ninapenda kusema nieleweke tangu mwanzo kuwa binafsi siandiki mambo haya kwa kujifurahisha, kulalamika au nikiwa na mtazamo wa kuunga mkono kambi yoyote, kati ya mbili kubwa ambazo zimejiainisha kuwa na upinzani kwa sasa.
Ninasema kuna kambi mbili kubwa na ambazo tayari zimejiainisha rasmi kwa sasa kuwa ndizo zenye upinzani mkubwa katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu.
Kambi hizi mbili, ile ya chama tawala, CCM na mgombea wake, Dk John Magufuli na Ukawa, kwa maana ya umoja wa vyama vinne vya upinzani na mwakilishi wao, Edward Lowassa zinaendesha kampeni zake, ambazo sote tumeziona, ingawa tunaweza kuwa tumeanza kuona kasoro chache, ambazo hata hivyo nikipata nafasi nitazizungumzia baadaye.
Ni wajibu wangu, nikiwa mwanataaluma, tena wa siku nyingi, mzoefu kusema kwamba lazima niweke kando ushabiki mwingi ulioanza kujitokeza kati yetu na kuwasumbua baadhi yetu kwa kiasi kikubwa, iwe ndani ya vyumba vyetu vya habari au kokote kule katika jamii tunamoishi au kufanya kazi.
Ni dhahiri tukumbuke kuwa kama waswahili wasemavyo, lisemwalo lipo, kama halipo, basi linakuja.
Nami, kama wanahabari, ninatambua kuwa tuna wakati mgumu hasa wa kujipambanua ili kujiepusha na kitanzi hiki, hata kama ni kigumu kiasi gani.
Tuna wakati mgumu wa kujiepusha na vishawishi vingi vya aina mbalimbali, vikiwamo vya fedha, ahadi lukuki na za aina tofauti, kama vyeo au madaraka iwe kutoka kwa wagombea au wapambe wao, kwamba endapo wataingia madarakani baada ya uchaguzi huo wa Oktoba 25, basi watatukumbuka.
Hilo wala siyo siri linajitokeza, liliwahi kujitokeza miaka michache iliyopita, hasa wakati ule wa kampeni kamambe zenye hisia zilizomwingiza madarakani Rais Jakaya Kikwete, kiongozi anayemaliza muda wake.
Tunaweza kuwa tumesahau, kampeni za Kikwete, mvuto aliokuwa nao, viliwachanganya wengi hadi leo.
Wakati ule kulikuwa na ushabiki mwingi na mkubwa wenye kishindo, ambao umeanza kujitokeza hata wakati huu wa kampeni za uchaguzi mkuu, hasa kwa ngazi ya urais zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini.
Wakati ule, mwaka 2005, wapo wanahabari kati yetu au miongoni mwetu waliotuhumiwa kwamba walikuwa wakimpendelea mgombea huyo wa CCM kwa sababu zile zile, zinazojitokeza leo kwa wagombea fulani fulani, zile zilizodaiwa kuwa hatimaye zingewawezesha wanahabari kulipwa fadhila.
Inawezekana, fadhila hizo zilitokea na kuonekana wazi wazi bila kificho, kiasi kwamba wapo wenzetu, hata kama wachache, ni wanataaluma wenzetu, ambao walitakiwa kuwa mfano katika jamii, lakini kwa bahati mbaya walijisahau na kugeuka kuwa wasemaji wa wagombea.
Matokeo yake, wao wamenufaika kwa kiasi kikubwa na mchango wao huo mkubwa katika kupiga debe au kuhakikisha mgombea wamtakaye anaingia madarakani na hilo lilikuwa kwa masilahi yao binafsi, wala si vyombo vya habari walivyokuwa wakivitumikia au hata kuvimiliki.
Kwa bahati mbaya, kuna hisia kama hizo, zimeanza kuzuka tena, zinasambaa kama moto wa kiangazi na hazifichiki tena kwamba miongoni mwetu imepenyezwa rupia.
Waswahili husema, penye udhia penyeza rupia, wanahabari tunapiga kampeni, tunashangilia wagombea, tena waziwazi, inashangaza.
Baadhi ya sababu za tuhuma kama hizo za wakati ule zimekuwa zikijionyesha dhahiri hata sasa kwenye maandiko yetu, michoro yetu ya vibonzo au katuni.
Ni ushahidi huo ambao upo dhahiri, pasi na shaka, unaonyesha kuwapo kwa fungamano linalokinzana na misingi ya taaluma yetu, ambayo ni pamoja na kujiendesha kwa weledi, bila ushawishi wa aina yoyote.
Hakuna shaka , sisi wanahabari, tukiwamo wahariri au mameneja na wengineo tunaobeba dhamana ya mamlaka ya kuamua kipi kiandikwe au kutangazwa wakati huu wa uchaguzi, kwa hakika tupo kitanzini.
Kitanzi hiki kibaya ambacho wakati mwingine ni cha kujitakia wenyewe kwa sababu ya umasikini wetu wa kipato au fikra kinatokana na baadhi yetu kuwa kuendekeza njaa zetu na matumaini ya muda mfupi.
Inasikititisha kuona sisi wanahabari tukianguka katika mitego ya wanasiasa, watu ambao siku zote wamekuwa wakituambia kuwa wao hawana adui wa kudumu.
Bila kujitambua, sisi kama wanahabari badala ya kutumia weledi wetu ipasavyo, tunaimba nyimbo zao wanasiasa, tunawalamba viatu, hata kama vitakuwa ni vichafu kiasi gani. Ni kwa kiasi kikubwa kwamba tunajishushia hadhi katika jamii kiasi kwamba heshima yetu ipo shakani, hasa inapotokea kuwa tunajikuta kwa sasa tumegeuka mashabiki , wapigadebe au wapuliza filimbi wakubwa wa wagombea, jambo ambalo linakiuka misingi ya taaluma yetu.
Tunavaa skafu, kofia au fulana na vitambulisho vya majina ya wagombea, vitu ambavyo tulitakiwa kujiepusha navyo kama kanuni zinavyotaka, lakini tumefumba macho, tumejisahau.
Inaumiza, inashangaza sisi kama wanataaluma ambao tumeweka misingi ya namna ya kuendesha mambo yetu, tunajikuta njiapanda tumekengeuka, hatukumbuki kanuni au hata sera zetu ambazo baadhi ya vyombo vyet vya habari zinavyo, zile zinazosema au kuelekeza ni kitu gani tufanye , nini mienendo ya kazi zetu, hasa wakati huu wa uchaguzi?
Hili linatokea, ni bahati mbaya kuwa miaka michache ya nyuma Baraza la Habari Tanzania (MCT) liliandaa miongozo ya namna ya kuandika habari za uchaguzi, ambayo iliheshimiwa na kuzingatiwa kwa kiasi kikubwa.
Inaelekea semina zote zilizoandaliwa mwaka huu, kabla ya kuanza kwa kampeni, ama zilikuwa maalum kwa ajili ya kuhalalisha pengine ulaji iwe kwa wahariri , mameneja wa vyombo vya habari au waandishi, matokeo yake, baadhi ya vyombo vyetu kwa sasa vimegeuka vijiwe vya wanasiasa tunaowabeba, tunaowasifu, bila aibu wala sababu za msingi.
Nilisema awali, kuwa kitu kinachoniumiza roho ni tuhuma nzito ambazo zimekuwa zikitolewa na kusambazwa iwe katika mitandao, kusikika katika mazungumzo na kwenye vijiwe karibu kote nchini kuwa baadhi yetu (wanahabari) tumehongwa, sijui ni ni fedha nyingi kiasi gani zimetufumba macho kiasi hiki cha kulazimika kuwapigia debe wagombea?
Hili ni jambo zito ambalo sisi kama wanataaluma ni lazima tuwe makini, tuliangalie, hasa wakati huu ambao kampeni zinaendelea. Nikiachana na wanahabari kupiga debe, natambua kuwa vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi vilisaini na kuridhia mwongozo wa maadili yanayohusu uchaguzi wa mwaka huu. Mwongozo huo, ambao ninaamini kila chama cha siasa kinao, umeweka miongoni mwake masharti ambayo lazima vyama vizingatie wakati wa kampeni.
Miongoni mwake ni kuweka picha za wagombea katika baadhi ya maeneo, mijini na vijijini, jambo ambalo limeanza kuzusha malalamiko kutoka kwa wanasiasa, wakiwamo wagombea.
Niishauri Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iwakumbushe wagombea au wapigadebe wazingatie maadili ambayo yalifikiwa na tume hiyo, Julai 27.   
/Mwananchi.

No comments :

Post a Comment