dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, September 8, 2015

SPIKA WA BUNGE MHE. ANNE MAKINDA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA TUME YA UTUMISHI YA BUNGE LA NIGERIA OFISINI KWAKE LEO!

Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda, (kulia), akiongea na Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria walipomtembelea leo Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo Septemba 6, 2015. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge ambapo Mhe. Makinda aliambatana na wajumbe wa Tume ya Bunge la Tanzania. Kulia kwake ni Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako. Bunge la Tanzania leo kwa lengo la kujifunza
Mh. Anne Makinda akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo
Kiongozi wa Msafara wa Ujumbe kutoka Tume ya Utumishi ya Bunge la Nigeria Mhe. Yepwi Stephen Dako akiuliza namna ambavyo Tume ya Bunge la Tanzania husimamia Watumishi wa Bunge la Tanzania katika kuleta ufanisi kazini wakati walipokutana na wenyeji wao kutoka Tanzania leo. Ujumbe huo wa tume ya Nigeria upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na Uendeshaji wa Bunge.
Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Ajira na Maendeleo ya Watumishi ya Tume ya Utumishi ya Bunge Mhe. Salehe Pamba akifafanua baadhi ya hoja zilizokuwa zikiulizwa na wajumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria (hawapo pichani) waliotembelea Bunge leo kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge.
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwa katika picha ya Pamoja na Ujumbe wa Tume ya Utumishi kutoka Bunge la Nigeria na wenyeji wao kutoka Bunge la Tanzania mara baada ya kukutana nao Ofisini kwake leo. Ujumbe huo upo nchini kwa lengo la kujifunza masuala mbalimbali ya Utumishi na uendeshaji wa Bunge.
. Spika wa Bunge ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi ya Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiagana na Kiongozi wa Msafara wa Tume hiyo Mhe. Yepwi Stephen Dako baada ya kumaliza mazungumzo yao.

(Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge)

No comments :

Post a Comment