dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, September 8, 2015

Tanesco hamjatenda haki, mngetoa taarifa mapema.

NA EDITOR

8th September 2015

Katuni.
Shirika la Umeme nchini (Tanesco), juzi lilitangazia umma kwamba nchi nzima itakuwa gizani kwa takriban wiki nzima kuanzia jana.
 
Shirika hilo lilieleza kuwa hali hiyo inatokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi inayozalisha umeme kutoka Songosongo mkoani Lindi.
 
Tanesco ilifafanua kuwa imechukua hatua hiyo kutokana na kazi ya kuunganisha bomba la gesi kutoka Mtwara na mtambo wa umeme wa Kinyerezi II.
 
Aidha, hali ya umeme ilitarajiwa kuwa mbaya zaidi jana kwa kuwa mitambo yote ya kuzalisha nishati hiyo ilikuwa inatarajiwa kuzimwa ili kufanikisha kazi hiyo.
 
Tunaamini kwamba dhamira ya Tanesco ni njema na imelenga kuboresha utoaji huduma umeme nchini ambayo kwa miaka nenda rudi, imekuwa haikidhi matarajio ya wateja wake na Watanzania kwa ujumla.
 
Hata hivyo, sisi hatuamini kuwa hatua ya Tanesco ya kuunganisha bomba la gesi kutoka mkoani Mtwara na mitambo yake, imekuwa ni ya dharura kiasi cha kulazimika kutoa taarifa kwa umma siku moja kabla.Tunasema na tuna imani kwamba mpango wa shirika hilo wa kuunganisha bomba hilo na mitambo ya Kinyerezi, haukuibuka ghafla tu juzi na hivyo kulazimika kuwapa wateja wake notisi ya muda mfupi, bali lilijipanga kwa kwa muda mrefu kwa kazi hiyo pasipo kukurupuka.
 
Kwa msingi huo, menejimenti ya Tanesco ilipaswa kutoa tahadhari mapema kwa wateja wake juu ya kuwapo kwa hatua ya kuzima mitambo yake ili kuwawezesha kujipanga kukabiliana na tatizo hilo.
 
Ni dhahiri kwamba mamilioni ya watu nchini, hutegemea nishati ya umeme kwa shughuli mbalimbali za kila siku za kujiongezea kipato pamoja na viwanda.
 
Mathalani, ukiachilia mbali viwanda ambavyo kwa asilimia kubwa hutegemea umeme wa Tanesco, lakini pia wajasiriamali mbalimbali hutegemea nishati ya umeme kuendeshea shughuli zao za kiuchumi kama vile saluni za kike na kiume, inateneti, gereji za magari, wauzaji wa vinywaji baridi na vikali, wauza samaki na nyama, mama ntilie, wachomeleaji vyuma; kutaja baadhi.
 
Kwa msingi huo, ni jambo lililo wazi kwamba hatua hii ya Tanesco kwa kiasi kikubwa itaathiri shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii ambazo kwa kiasi kikubwa zinategemea nishati ya umeme.
 
Ni kutokana na hilo, ndipo tupoona umuhimu wa Tanesco ingepaswa kutoa taarifa ya kukosekana kwa umeme mapema zaidi ili makundi hayo yote yajiandae vya kutosha.
 
Kimsingi, Tanesco haikuwatendea haki wateja wake na umma wa Watanzania kwa kufanya uamuzi huo wa ghafla wa kuzima mitambo yake bila kujali athari watakazokumbana nazo.
 
Aidha, hatua hii ya Tanesco kwa kiasi kikubwa pia itaathiri uzalishaji wa viwandani kwani vitalazimika kuingia gharama za kutumia majenereta yanayotumia mafuta.
 
Matumizi ya jenereta, ni wazi kwamba yatachangia kwa kiasi kikubwa kupandisha bei ya bidhaa zinazozalishwa viwandani na hivyo kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi.
 
Viwanda vingi vinaendeshwa kwa bajeti na hatua hii ya Tanesco kuzima ghafla mitambo yake, italeta athari kubwa.
 
Mbali na shughuli hizo za kiuchumi, lakini pia kuna masuala ya kijamii kama shughuli za hospitali kwani kwa hatua hii ya Tanesco, ni dhahiri wagonjwa wengi wanaohitaji huduma za matibabu wataathirika.
 
Ikumbukwe kuwa Tanzania kwa sasa inapigania kupeleka watu wake kwenye uchumi wa kati, na kwa msingi huo suala la nishati ya umeme, ni muhimu kwa watu wa kipato cha chini wanaotaka kuinua hali zao za maisha.
 
Kwa hakika Tanesco inapaswa kukubali kwamba haikuwatendea haki wateja wake na umma wa Watanzania kwa hatua yake hii.
 
Hata hivyo, sisi hatupingi dhamira njema ya Tanesco kuboresha miundombinu ya umeme nchini, tunachosisitiza ni kwmaba yalipaswa kuwapo mawasiliano bora na ya mapema ambayo yangesaidia wananchi kujipanga vizuri na athari za makali ya kukatwa kwa umeme.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment