dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, September 9, 2015

Wanawake wanaougua kansa ya kizazi wamwagiwa neema.

Baadhi ya wageni waalikwa na akina mama wanaotibiwa ugonjwa wa kansa ya kizazi katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati taasisi zisizo za kiserikali za Vodacom Foundation, T-Marc Tanzania na Pink Ribbon Red Ribbon zikitangaza mfumo wa kuwasaidia matibabu jana. PICHA: FREDDY MARO WA IKULU
Taasisi tatu nchini, zimejipanga kusaidia gharama za matibabu kwa wanawake wanaougua kansa ya kizazi hususani wenye maisha duni na waishio vijijini.
Taasisi hizo ni Vodacom Foundation ,T-Marc Tanzania na taasisi ya kimataifa ya Pink Ribbon Red Ribbon.
 
Taasisi ya Vodacom imetoa Dola 87,400 za Marekani kwa kuwawezesha wanawake wanaosumbuliwa na kansa ya kizazi kusafiri kutoka maeneo wanayoishi hadi jijini Dar es Salaam ilipo Taasisi ya Uchunguzi na Matibabu ya Kansa ya Ocean Road (ORCI) kufanyiwa uchunguzi wa awali na matibabu.
 
Msaada huo kwa kuanzia utawalenga wanawake wanaoishi sehemu ambazo taasisi ya Pink Ribbon Red Ribbon inaendesha miradi yake ya mikoa ya Iringa, Mbeya na Mwanza.
 
Katika ushirikiano huo, T-Marc itawapatia walengwa kwa ushirikiano na taasisi za afya kwenye mikoa hiyo ambapo baada ya kupatikana, wataunganishwa na mabalozi wa mradi huo kutoka taasisi ya Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT).CCBRT watapatiwa fedha za kusafirisha walengwa kutoka T-Marc kwa njia ya M-Pesa kununua tiketi za usafiri na watakapofika jijini Dar es Salaam, watapokelewa na ufuatiliaji, gharama za uchunguzi  na za matibabu yao, yatafanywa na T-Marc.
 
Aidha, T-Marc itahakikisha pia wamalizapo uchunguzi na matibabu, wanarejeshwa makwao.
 
Huduma hiyo pia itatolewa kwa wagonjwa watakaopenda kutibiwa katika Hospitali ya Bugando ya jijini Mwanza ambayo itaanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa kansa  karibuni.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliofanyika jana katika Taasisi ya Ocean Road, Meneja wa Miradi wa T-Marc,  Doris Chalambo, alisema tayari umehudumia wanawake 17 kutoka mikoa ya Iringa na Mbeya.
Alisema Tanzania pia ni nchi yenye vifo vingi vya kansa barani Afrika.
 
“Kupitia msaada huo wa Vodacom Foundation na Pink Ribbon Red Ribbon, wanawake wote waliojitokeza kuchunguzwa na kukutwa wameathirika kwa kiasi kikubwa, wanaendelea kusaidiwa gharama za matibabu,” alisema.
 
Kwa upande wake, Mkuu wa Vodacom Foundation, Renatus Rwehikiza, alisema msaada wa Dola za Marekani 87,400 umelenga kusaidia matibabu ya akina mama na kupunguza vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa kansa ya kizazi 
 
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ocean Road, Beatrice Erasto, alisema wananchi wengi wameanza kuuelewa ugonjwa huo na wanajitokeza kwa wingi kufanyiwa uchunguzi wanapohisi dalili tofauti na awali.
Alitoa wito kwa akina mama wenye umri wa kati ya miaka 30 na 50 kujitokeza kufanyiwa uchunguzi wanapohisi dalili ya ugonjwa huo kwani ukigundulika mapema, rahisi kutibika.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment