dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 14, 2015

Rais Kikwete aonya wanaopanga kulinda kura vituoni

Rais Jakaya Kikwete
By Sauli Giliard, Mwananchi Digital
Rais Jakaya Kikwete amesema watu wanaopanga kubaki katika vituo vya kupigia kura baada ya kumaliza zoezi hilo kwa lengo la kulinda kura kunaashiria uvunjaji amani, hivyo serikali imejipanga kupambana na hali hiyo siku ya uchaguzi.
Rais amesisitiza kwamba wanaopaswa kulinda kura ni mawakala pekee na si wafuasi wa mgombea ama vyama.
Akizungumza leo katika sherehe za Kilele cha Mwenge wa Uhuru zilizofanyika  Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kiongozi huyo anayemalizia muda wake madarakani amesema viongozi wanaowaagiza wafuasi wao kulinda kura wana nia mbaya dhidi ya amani ya nchi.
“Mnatakiwa muondoke kwenye vituo baada ya kupiga kura….kura utazilindaje? Mawakala ndio pekee wanaoweza kulinda. Mkikaidi hilo, hatutawavulimia. Serikali imejipanga kupambana na wale wote watakaokaidi agizo la Tume ya Uchaguzi (NEC),” amesisitiza Rais Jakaya Kikwete.
Katika shehere hizo za mwenge zinazoendana sambamba na maadhimisho ya siku ya kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais Kikwete amewataka Watanzania kuchagua watu waadilifu ambao dhamira ya kupambana na rushwa kwa vitendo.
“Tumchague mtu ambaye hana ukabila, udini na ubaguzi wa rangi…tumchague kiongozi atakayetetea maslahi ya makabila yote 126,” amesema rais huku akimnukuu Mwalimu Nyerere aliyefariki miaka 16 iliyopita.
Sherehe hiyo imehudhuriwa pia na Spika wa Bunge anayemaliza muda wake, Anne Makinda, wakuu wa mikoa na viongozi wengine wa ngazi tofauti serikali na kupambwa na nyimbo za makabila na wanafunzi wa shule mbalimbali mjini Dodoma.

No comments :

Post a Comment