dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, January 17, 2016

IELEWE KANUNI NAMNA YA KUEPUKA HASIRA

Kanuni ya 90 kwa 10 ni muhimu na itakusaidia katika huyabadili maisha yako na namna unavyoyapokea au kuyaangalia mambo na kuonyesha hisia zako.
Kanuni hiyo ina msingi ufuatao; asilimia 10 ya maisha yetu inafanywa na vile vitu vinavyotokea kwetu na tusivyoweza kabisa kuvibadili kwa uwezo wetu.
Asilimia 90 ya vyote vinavyotokea katika maisha yetu vinategemea jinsi tunavyoonyesha hisia zetu.
Kamwe hatuwezi kubadili chochote wala kugeuza chochote katika yale yanayotokea kwetu katika ile asilimia 10% mfano, hatuwezi kubadili wala kuzuia pale gari linapoharibika barabarani, hatuwezi kuzuia wala kubadili chochote pale ndege inapochelewa kuondoka uwanjani, hatuwezi kufanya chochote pale kitu kinapoingilia safari yako barabarani na kukuchelewesha, kwa mfano foleni isiyotarajiwa.
Asilimia 90 ni tofauti. Sisi tuna uwezo mkubwa katika kuiamua na kubadili hali kutegemea na vile tunavyozionyesha hisia zetu.
Huwezi kuzuia taa nyekundu inapowaka barabarani kukuashiria usipite, lakini waweza kuzitawala hisia zako zinazoweza kusababishwa na taa ile.
Kamwe usimruhusu mtu au watu wakupumbaze au kukufanya mjinga kwa kuzichochea hisia zako. Jaribu kujitawala na kujiweza.
Labda tutumie mfano huu; Unapokunywa chai asubuhi na familia yako mara binti yako anagonga kikombe kwa bahati mbaya na chai inamwagika na kuchafua shati lako la jeupe la kazini.
Hapa kwa kweli huna lolote la kufanya kuhusu kilichotokea, (maji yamekwisha mwagika), kinachofuata sasa kitategemea na utakavyozionyesha hisia zako. Je, utalaani, utatukana, utabwata, utampiga makofi binti yako? Kama utamchapa, baada ya hapo labda pia utamgeukia mke wako na kumgombeza kwa kuweka kikombe vibaya mezani na hapo mtaanza kuzozana na mkeo.
Mara utaenda chumbani kubadili shati na kwa hasira utatoka na kumkuta binti yako akiendelea kulia na kwa kulia na kutokunywa chai anaachwa na gari la shule. Labda mke wako hawezi kumpeleka binti yako shuleni, kwa hiyo unalazimika kumchukuwa kwa hasira kumuwahisha shuleni, kwa sababu umechelewa unaendesha kwa kasi kiasi cha kusimamishwa na askari wa barabarani na kutozwa faini.
Baada ya kucheleweshwa zaidi na askari mnafika shuleni na mwanao mmenuniana na kwa hasira anaruka kutoka kwenye gari bila hata kukuaga na kukimbilia dasani.
Unatoka na kukimbia ofisini, mara unapoingia ofisini unakumbuka umesahau begi lako la ofisini, kwa sababu ulitoka chumbani kwa hasira. Siku yako imeanza vibaya, itaendelea vibaya na kuwa mbaya zaidi hata mwisho wake.
Unaporudi numbani unakuta mama na binti wote hawana amani na wewe, kwa kile ulichokianzisha asubuhi.
Yote haya kwa nini? Ni kwa vile ulivyozionyesha hisia zako asubuhi.
Kwa nini siku yako imekuwa mbaya?
Je, ni chai imesababisha?
Je, ni binti yako amesababisha?
Je, ni askari wa barabarani?
Au ni wewe uliyesababisha?
Ukweli ni kwamba hukuwa na lolote la kufanya kwa kumwagika kwa chai, lakini jinsi ulivyoonyesha hisia katika zile sekunde tano, ndipo ulipoharibu siku yako. Yamkini ingekuwa bora ungefanya tofauti kama ifuatavyo.
Chai imemwagika katika shati lako la kazini,
Binti yako anataka kulia kwa hofu
Taratibu mguse begani na kumwambia asihofu kwa sababu hali kama hizo hutokea, ila awe makini wakati mwingine awapo mezani.
Chukua taulo haraka jifute na kubadili shati na utoke na begi lako la kazini na kuagana na binti yako akienda kupanda gari la shule.
Ondoka, wahi kazini na upate dakika chache za kusalimiana na wafanyakazi wachache kabla ya kuanza kazi.
Angalia tofauti hapa!
Imekuwa michakato miwili tofauti, yote ilianza kwa tukiko moja, na yote imeishia katika hali za tofauti.
Kwa nini? Kwa sababu ya jinsi ulivyoonyesha hisia zako.
Hapa utaona ukweli kwamba, una nafasi kubwa ya kuzitawala asilimia 90 za yale yanayoendelea maishani mwako, hususan kwa jinsi uzitawalavyo hisia zako.
Jinsi ya kuitendea kazi kanuni hii
Iwapo mtu au watu wanakusema au kukufanyia mambo mabaya, usiyameze na kuyaruhusu yakuumize.
Yaruhusu yakutoke haraka kama vile maji yanavyoachana na glasi.
Usiziruhusu semi mbovu ziumize moyo wako. Onyesha hisia zako kiusahihi na kwa kufanya hivyo hautaiharibu siku yako.
Kwa kuonyesha hisia zetu vibaya twaweza kupoteza marafiki, twaweza kufukuzwa kazi, twaweza kuharibu jina na sifa yetu au kujiongezea msongo wa mawazo.
Unafanyaje pale mtu anapokuendeshea gari vibaya au kukuchomekea ukiwa barabarani unaendesha, unatukana? unalaani? Unagonga usukani au kupiga honi kwa hasira? Je, unapofanya hivyo kuna anayekujali? Kwa nini uruhusu magari yaharibu raha ya uendeshaji wako. (usisahau kanuni ya 90-10). Umeambiwa unafukuzwa au unapunguzwa kazi, kwanini upoteze usingizi na kukaa ukihofu? Inawezekana kubadili hiyo hali.   

No comments :

Post a Comment