dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 15, 2016

Afya wapokea magari 58 ya wagonjwa!

IMEANDIKWA NA LUCY LYATUU /Habari Leo.


WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea msaada wa magari 58 yakiwemo ya kubeba wagonjwa.

Mengine ni ya kuratibu shughuli za huduma za afya ya mama na mtoto ya thamani ya zaidi ya Sh bilioni 5.4 katika mikoa sita ya Kanda ya Ziwa nchini. Msaada huo umetolewa na mashirika ya Afya Duniani (WHO) magari 50; na Shirika la Kimataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) magari manane.

Magari hayo yamekabidhiwa kwa wabunge wa mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Kagera, Mwanza, Mara, Simiyu, Geita na Kigoma.

Akizungumza jana Dar es Salaam wakati akikabidhi magari hayo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema msaada huo utawezesha serikali kufikia malengo yake ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi pamoja na kuzuia vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga kutoka vifo 432 hadi 292 katika vizazi hai 100,000.Aidha Ummy aliyashukuru mashirika ya WHO na UNFPA kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabali watanzania, ikiwemo vifo vya wajawazito na watoto wachanga.

Waziri Ummy aliwataka wabunge, wakurugenzi na waganga wakuu wa wilaya, magari hayo yatumike ilivyokusudiwa na yasihusike kubeba maofisa kutoka eneo moja kwenda lingine.

Kwa upande wake Mbunge wa Maswa Mashariki, Stanslaus Nyongo alishukuru kwa msaada huo wa gari katika jimbo lake na kwamba utasaidia kuimarisha huduma za afya ili kudhibiti vifo vingi vya wanawake na watoto.

Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA, Dk Hashina Begun alisema wametoa msaada huo kama njia mojawapo ya kushiriki katika kuimarisha huduma za afya nchini ili jamii ya wanaohitaji waweze kufikiwa na kupata huduma.

Alisema msaada huo ni moja ya utekelezaji wa mpango wa shirika hilo kwa Tanzania kwa ajili ya kuboresha huduma za afya nchini kuanzia katika vituo vya afya ili kutoa huduma ya afuya yenye ufanisi.

Mwakilishi Mkazi wa WHO, Dk Grace Saguti alisema magari hayo yametolewa kwa ajili ya kusaidia kuboresha huduma za afya ikitegemewa kupunguzwa kwa vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga nchini.

No comments :

Post a Comment