dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 25, 2016

NDOA YA UPEPO YAFUNGWA TENA JIJINI MBEYA!

Bwanaharusi Ndugu Samwel Makalobo akivishwa pete ya ndoa na Mke wake Given Mgaya katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Isanga jijini Mbeya .Picha na Keneth Ngelesi . 

Bwanaharusi akisaini hati ya Ndoa mbele ya mchungaji wa kanisa hilo Ndugu Mathias Mwaijungu mara baada ya ndoa hiyo kufungwa rasmi Desemba 23 mwaka huu.

Bibi harusi akisaini hati ya Ndoa mbele ya mchungaji wa kanisa hilo Ndugu Mathias Mwaijungu mara baada ya ndoa hiyo kufungwa rasmi Desemba 23 mwaka huu.

HATIMAYE lile tukio lililovuta hisia za watu wengi la bibi harusi, Given Mgaya, kukimbiwa kanisani na mchumba wake siku ya harusi, limepatiwa jibu baada ya bwana harusi , Samwel Mwakalobo, kujirudi na kuamua kutimiza ahadi yake ya kufunga ndoa.

Ndoa hiyo imefungwa leo majira ya saa tisa Desemba 23 katika Kanisa la (K.K.K.T) Usharika wa Isanga na kufungishwa na Mchungaji, Mathias Andangile Mwakijungu, huku tukio hilo likishuhudiwa na idadi kubwa ya waumini na wananchi wa kawaida waliojitokeza kanisani hapo.

Kabla ya maharusi hao kula kiapo cha ndoa,Mchungaji Mwaijungu alitumia zaidi ya saa moja kutoa nasaha kwa maharusi kutokana na tukio lilotokea awali Disemba 16 mwaka huu baada ya Bwana harusi kuingia mitini bila kutoa sababu zozote.

Mbali na kutoa nasaha kwa maharusi,pia Mchungaji Mwaijungu alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya waumini na watu wengine kuacha tabia ya kueleza mambo yasiyo yajua tena bila kuwa na uhakika.

Alisema tabia hiyo huenda ndiyo iliyosababisha tukio la kukwama kufungwa kwa ndoa hiyo baada ya baadhi waumini na watu wengine kwa maslai yao walimua kueleza uzushi ulio iibua taaruki kubwa.

Baada ya nasaha hizo na kunukukuu baadkitakatifu cha Bihi ya maandiko kutoka kitabu Biblia ndipo ulipo fika muda kwa maharusi hao kutimiza ahadi ya kula kiapo cha uaminifu katika ndoa yao.


/Chanzo: JamiiMojaBlog,Mbeya

No comments :

Post a Comment