dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 25, 2016

Papa Francis: Ataka amani baina ya Israel na Palestina!


Papa Francis ametoa wito kufanywe juhudi mpya kuleta amani baina ya Waisraeli na Wapalestina.

Katika hotuba yake ya Krismasi, aliyotoa Vatikani, Papa alizihimiza pande mbili zinazohusika, kujaribu kuazimia kuandika ukurasa mpya na kumaliza chuki na kulipizana kisasi.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki pia ametaka kumalizwa kwa vita nchini Syria akisema ni wakati wa silaha kunyamazishwa.

Katika ujumbe wake wa Krismasi kiongozi wa kanisa la Anglikana duniani Askofu mkuu Justin Welby amewataka raia kumuomba Mungu ili kukabiliana na ugaidi.

Aidha amesema kuwa mengi yanapaswa kufanya ili kukabiliana na ukosefu wa usawa.

No comments :

Post a Comment