dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 25, 2016

Rais Magufuli kula Christmas Singida!



Leo ni sikukuu ya Krismasi, ambapo wakiristo wa Tanzania wanaungana na wenzao duniani kote kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Yesu Kristo yapata miaka 2000 iliyopita.

Katika siku hii, waumini wa madhehebu ya kikristo wanahudhuria ibada ya krismasi makanisani na kupokea ujumbe na mafundisho ya dini hiyo kuhusu umuhimu wa krismasi kwa maisha ya binadamu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, yuko mkoani Singida ambako yeye na mkewe Mama Janeth wanatarajia kuungana na waumini wengine wa dini ya Kikristo katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ambaye alimlaki Rais Magufuli jana alipowasili mjini Singida, amewaomba waumini wa dini ya kikristo mkoani Singida kujitokeza kwa wingi kuungana na Rais Magufuli katika ibada ya Krismasi kwani imekuwa ni heshima kwao kutokana na uwepo wa Rais Mkoani Singida kwa ajili ya sikukuu ya Krimass.

No comments :

Post a Comment