dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 30, 2016

Tumeanza kupiga hesabu za 2020- Chadema!


Kigoma. Chadema mkoani Kigoma imeanza kujipanga kwa ajili ya kufanikiwa katika chaguzi zijazo, lengo likiwa Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo, Ally Kisala amesema chama hicho kina mpango wa kujenga tawi na kuweka msingi katika kila mitaa na vijiji ili kushinda mwaka 2020.

Kisala amesema lengo la mkakati huo ni kushindana na CCM yenye mabalozi wa nyumba kumi na matawi katika mitaa na vijiji vingi nchini.

“Tunaanza uchaguzi wa chama mwezi ujao (Januari, 2017) na tumehamasisha jamii hasa watu wenye kukubalika waje kugombea uongozi kuanzia ngazi ya chini Chadema,” amesema Kisala.Kuhusu chama hicho kuporomoka kisiasa mkoani Kigoma na kupoteza jimbo la Kigoma Kaskazini na Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji waliyoongoza kati ya mwaka 2010 hadi 2015, amesema wanajipanga kurudisha madaraka.

“Tunakiri kupoteza jimbo na manispaa, lakini tumejipanga, watu wataona nini tutafanya mwaka 2019 na 2020 kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu,” Kisala amesema.

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Omary Gindi amewataka baadhi ya viongozi kuacha woga wa kukitetea chama hadharani.

/Mwananchi.

No comments :

Post a Comment