BIDHAA mbali mbali ambazo ni muhimu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, zikiwa tayari zimeshanunuliwa na wachuuzi ndani ya mnada katika soko la Matunda Chake Chake, zikisubiri kusafirishwa na kupelekwa Unguja.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA
DALALI katika Mnada wa soko la Matunda Chake Chake aliyejulikana kwa jina la Khamis, akionyesha maboga ambayo yananadiwa na fungu la maboga manne liliuzwa 15000/=.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
BIDHAA za ndizi aina ya Mkono Mmoja zikiwa zimetundikwa katika soko la Matunda Chake Chake, Mkungu mmoja wa ndizi hizo zinauzwa kati ya shilingi 40000/= hadi 35000/= na dole moja linauzwa kati ya shilingi 2000/= hadi 1500/=.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
NDIZI aina ya Alhasan ambayo imeuzwa shilingi 73000/= katika mnada wa soko la matunda Chake Chake, ni miongoni mwa ndizi ambazo zimekuwa na bei katika wmezi mtukufu wa Ramadhani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).
No comments :
Post a Comment