Mwanariadha maarufu duniani kutoka Jamaika, Usain Bolt amepata ofa kujiunga na klabu ya soka ya Ligi daraja la kwanza nchini England ya Burton Albion baada ya kutangaza kustaafu akiwa kwenye mashindano ya Riadha ya Dunia yaliyomalizika London wiki iliyopita Jumapili.
Kocha wa Burton Albion, Nigel Clough amesema anafahamu rekodi ya mwanariadha huyo ambaye amewahi kucheza soka wakati akiwa mdogo hivyo amempa muda wa kutafakari kuhusu ofa ya kujiunga na klabu hiyo.“Nina uhakika tutampata mwanariadha huyo kwa ajili ya majaribio kwani anaonekana mwenye nguvu na mbio na sisi tunataka wachezaji kama yeye hii sio hadithi hebu angalia Mwanariadha kama Adam Gemili ni mwanariadha mwenye mafanikio kwenye mbio za 4x100m alicheza mpira kabla ya kuanza kukimbia, Navutiwa sana kufanya nae kazi kwani ni vitu vichache tu vya kumbadilisha awe mchezaji kamili wa mpira wa miguu”,amesema Nigel Clough juzi kwenye mkutano na waandishi wa habari kabla ya mechi kati Burton Albion na Middlesbrough.
Usain Bolt amestaafu riadha kwa fedheha baada ya kufanya vibaya kwenye mbio za miata 100 na 400 alizokimbia kwenye mashindano hayo na kuishia nafasi ya tatu.

No comments :
Post a Comment