dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 22, 2017

Gobless Lema: Familia ya Lissu ni Watanzania!

Mbunge wa Arusha Mjini Gobless Lema amemjibu Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuhusu kauli aliyotoa jana kuwa serikali ipo tayari kumtibu Lissu endapo familia yake itaomba kwa serikali, Lema amesema kuwa familia ya Lissu hajashindwa kumgharamia matibabu.

Lema amesema kuwa anaamini familia ya Tundu Lissu ni Watanzania wote ambao wanapenda haki na Demokrasia ndani ya nchi, na wote ambao wanaumizwa na jambo hilo bila kujali itikadi zao hivyo watachanga shilingi moja moja kwa ajili ya matibabu ya Tundu Lissu na hata ikibidi mali zao watauza ili kuweza kumuwezesha Tundu Lissu kupata matibabu."Familia ya Lissu ni Watanzania wote wanaopenda utawala wa sheria, Utawala wa Demokrasia, familia ya Lissu ni Watanzania wote bila kujali itikadi zao ambao wanajisikia vibaya kwa matendo ya kihalifu kwa wabunge kupigwa risasi hadharani na bunge lisichukue hatua stahiki hii ndiyo familia ya Lissu, mtu yoyote ambaye anaguswa na ubinadamu na familia hii haijashindwa kumlipia matibabu tutachanga shilingi moja moja ikiwa ni lazima sana tutauza hata mali zetu kuhakikisha kwamba Mhe. Tundu Lissu akosi fedha za matibabu" alisema Godbless Lema

Jana Septemba 21, 2017 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa Tanga alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia yeye imemuhakikishia Mhe. Tundu Lissu na familia kuwa ipo tayari kugharamia matibabu yake zaidi pindi tu watakapopata maombi kutoka kwao.

No comments :

Post a Comment