dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 29, 2017

Kesi za udhalilishaji Mjini Magharibi Unguja zapungua!

Kesi za udhalilishaji wanawake na watoto katika mkoa wa Mjini Magharibi Unguja zimepungua kuanzia Januari hadi Septemba 2017 ukilinganisha na mwaka jana.

Kesi hizo zilizokuwa zimeshika kasi kisiwani Zanzibar zimepungua kutoka 633 kipindi kama hicho mwaka jana hadi kufikia 404 mwaka huu.

Mratibu Msaidizi Dawati la Jinsia Wanawake na Watoto mkoani humo, Kassim Fadhil alisema hayo jana katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia yaliyofanyika Madema mjini Unguja.Alisema kasi ya kupungua vitendo hivyo imekuja baada ya ushirikiano kati ya wananchi, taasisi za kiraia na Jeshi la Polisi ambalo ni wahusika wakuu wa kupinga matendo hayo dhidi ya raia.

Mkurugenzi Msaidizi Dawati la Jinsia Wanawake na Watoto Mjini Magharibi Unguja, Zahor Khamis alisema kwamba wanadhamira kuweka vitengo maalumu vya usuluhisho na utoaji wa elimu ya kutosha kwa baadhi ya wanandoa watakaobainika kuwa na matatizo ya udhalilishaji.

No comments :

Post a Comment