dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 28, 2017

Raila Odinga asema ataapishwa Disemba!


Kiongozi wa Upinzani Kenya NASA, Raila Odinga amesema anatarajia kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo Desemba 12, mwaka huu ambayo itakuwa  siku ya uhuru wa Kenya.

Odinga ametoa kauli hiyo ikiwa katika uwanja wa Jacaranda saa chache baada ya Rais Kenyatta kuapishwa kuwa Rais katika uwanja wa Kasarani.

Hata hivyo, wakati Odinga akisema hayo, Rais Kenyatta mara baada ya kuapa amewaambia na wananchi wa Kenya kuwa hakutakuwa na shughuli zingine za uchaguzi na yeye ndiye Rais mteule wa Kenya.

Hata hivyo, Polisi nchini Kenya walivamia uwanja uliopangwa kufanyika mkutano na maombolezo ya wananchi waliofariki wakati wa vurugu za uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26, mwaka huu.

Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa leo kuwa Rais wa Kenya ili kuwatumikia wakenya katika muhula wa pili wa uongozi.

No comments :

Post a Comment