dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 29, 2017

Uingereza, Marekani wampa tano Uhuru Kenyatta!


Nairobi, Kenya. Muda mfupi baada ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake William Ruto kuapishwa jana, Marekani na Uingereza zilituma salamu za pongezi na zikaahidi kushirikiana na Kenya huku zikitoa wito wa kufanyika majadiliano kuondoa migawanyiko katika jamii.

Salamu za pongezi kutoka kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ziliwasilishwa na Waziri wa Masuala ya Afrika Rory Stewart aliyehudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Kenyatta na naibu wake na akasema tukio hilo la Jumanne ni fursa kwa Kenya kusonga mbele baada ya uchaguzi uliochukua muda mrefu.

Taarifa kutoka ofisi inayoshughulikia masuala ya Jumuiya ya Madola imesema Rais Kenyatta anakaribishwa kwenye mkutano wa Jumuiya hiyo utakaofanyika London mwakani.

“Huu ni wakati ambao Kenya inaweza kusonga mbele baada ya uchaguzi uliorefushwa, kusababisha migawanyiko na kuingia na ari mpya ya maridhiano,” alisema Stewart.

“Natumai kwamba Wakenya wote watatambua haja sasa ya kuingia kwenye mjadala wa kitaifa na kuponya makovu.”

Katika hatua nyingine, taarifa ya maandishi ya Marekani imesema inatarajia kuimarisha ushirikiano na kurejesha ushirikiano baina ya nchi mbili hizo katika miaka michache ijayo.

Serikali ya Marekani imeelezea wasiwasi wake kuhusu mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini na matumizi makubwa ya nguvu yasiyo ya lazima dhidi ya raia na imetoa wito wa kufanyika mjadala wa kitaifa kama sehemu ya mchakato wa kukabili mgogoro huo.

"Tunawahimiza Wakenya kuungana na kufanya majadiliano ya wazi, endelevu nay a haraka kwa ajili ya kuponya migawanyiko katika jamii,” imesema taarifa ya Marekani.

No comments :

Post a Comment