airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, December 30, 2017

ZANZIBAR-CANADIAN DIASPORA ASSOCIATION (ZACADIA) YAUKARIBISHA MWAKA MPYA KWA KISHINDO!



ZACADIA - Zanzibar-Canadian Diaspora Association, ambayo ni moja katika Jumuiya za Wazanzibari wanaoishi nchini Canada yenye makao makuu yake jijini Toronto, imesema leo kuwa inauanza mwaka mpya wa 2018 kwa mafanikio mazuri sana baada ya kufuzu kupeleka nyumbani Zanzibar katika mwezi huu wa December Container zima la futi 40 ambalo lilijazwa vitabu vya kila aina vyenye thamani zaidi ya shilingi bilioni mbili na nusu, pamoja na zana tafauti kwaajili ya matumizi ya hospitalini.

Hayo yalisemwa leo katika mkutano wa mwaka wa Jumuiya hio uliohudhuriwa na wanachama wake hapo Tobermory Drive #15, katika kitongoji cha North York, Toronto. 

Madhumuni ya mkutano huo ulikuwa ni kuweka road  map katika shughuli za Jumuiya hio kwa mwaka ujao pamoja na kujifunza kutokana na mapungufu ya mwaka unaomalizika.

Ilielezwa kwenye mkutano huo kuwa vitabu vipya vilivyopelekwa Zanzibar ambavyo vilikuwa zaidi ya vitabu 25,000 vilikuwa katika fani tafauti za taaluma, kama vile Pure Science, Agriculture, Ecology, Medicine, Business, Mathematics, Engineering Science and Social Studies.

Pia, zana tafauti zilizopelekwa Zanzibar ambazo zinategemewa kufika katika mwezi wa February zikiambatana na mabuku zilikuwa ni pamoja na:

1) Syringes - 30 mls, 10 mls, 5 mls

2) X-Ray Detectable Sponges

3) Trocar Thoracic Catheters

4) Brighton Epistaxis Balloons

5) Basic Cleansing Enema Bag

6) Infusion Sets “Smart Site”

7) C-Section Drape

8) MAX-Aero Chamber

9) Sterile Specimen bottles

10) Triumph LT Sterile Gloves

11) Tracheostomy Care Tray

12) T.E.D Anti-Embolism Stockings

13) Radiology Basic Tray

14) Gypsona Bandages

15) Safety Wings infusion sets

16) Sterile Lead Gloves

17) Suction Catheter with Whistle Tip

18) Hommark C80 N95 masks

19) Prickers

20) Gauze Dressing.


Pia, zilikuwemo wheelchairs pamoja na vitanda vya hospitali kwenye hilo Container lililotumwa Zanzibar.

Vice-President wa Jumuiya hio Shk Hassan Othman alitaja mafanikio makubwa ya Jumuiya hio kwa mwaka 2017 yalikuwa sio tu kupeleka vitabu zaidi ya 25,000; bali ni kule kuendelea kuendeleza ile tabia ya kuwapelekea msaada wa futari na Sikukuu/Idi watoto mayatima wa Unguja na Pemba kama inavyofanyika kila mwaka. 

Pia, Vice-President alielezea kuwa ZACADIA inamajivuno makubwa kutokana na namna Watanzania kutoka diaspora tafauti wanavyoitumia WorldRemit kupeleka pesa nyumbani. Alitaja kuwa zaidi ya shilingi bilioni 3 kila mwezi zinapelekwa nyumbani kupitia WorldRemit kutoka ughaibuni. 

Aliendelea Vice-President kusema kuwa, "Mafanikio haya yamepatikana kwasababu Wana-Zacadia tulikaa pamoja kuamua juu ya mustakbali wa nchi yetu juu ya hili suala la remittances na vipi linaweza kuengeza kipato cha foreign currencies kwa nchi yetu na tukasema tutaweza na kweli leo tumeweza. Kwahivyo, yapo mengi ambayo tutayaweza pia, lakini inahitaji tukae pamoja na tuamue kwa pamoja", alimalizia Vice-President.

WorldRemit ni kampuni ya kusafirisha pesa kiurahisi ya mtandaoni ambayo ilipelekwa Tanzania kupitia juhudi za ZACADIA.

Secretary wa Jumuiya na Member wa Board of Trustees Bi Arafa Mustafa aliwataka wananchama wote wapya kujitambua kuwa wapo nyumbani na kuwa kila mmoja anayohaki ya kugombea nafasi yoyote ile ya Jumuiya inapokuwa wazi. Pia, aliwataka wanachama kujipeleka mbele pale wanapohitajika kwa kazi za kujitolea za Jumuiya.

Akiufunga mkutano huo Mwenyekiti wa ZACADIA Shk Omar Said aliwatakia wanachama wote wa Jumuiya hio na Wazanzibari wote wanaoishi Canada na nyumbani pamoja na Watanzania wote kwa jumla mafanikio, furaha na amani katika maisha yao katika mwaka mpya ujao wa 2018.

Mwenyekiti alimalizia kwa kuwataka wanachama wote wa Jumuiya kuzidi kujitolea katika mwaka wa 2018 katika shughuli za ZACADIA kwa faida ya nchi yetu.

No comments :

Post a Comment