dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, July 23, 2018

Jukwaa la Katiba wataja mambo tisa yatakayofanikisha uchaguzi wa Haki!

Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) limeitaka Serikali kufanya marekebisho ya sheria na Katiba ya nchi yanayoendana na mahitaji ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 23, 2018 jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda ametaja maeneo tisa yanayohitaji mabadiliko ili kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru na wenye haki.

“Kutokana na kwamba serikali ya awamu hii imetamka kuwa mchakato wa katiba mpya sio kipaumbele chake, na kimesalia kipindi kifupi kufika mwaka wa uchaguzi tukiwa kama jukwaa la katiba tunashauri mabadiliko yafanyike haraka”, amesema Mwakagenda.Mwakagenda ametaja maeneo yanayohitaji mabadiliko ya katiba zaidi kuwa ni, uhuru kamili wa tume ya taifa ya uchaguzi na tume ya uchaguzi ya Zanzibar, kuungana kwa vyama vya siasa, uwakilishi wa uwiano wa 50/50, mgombea binafsi aruhusiwe kwenye uchaguzi mkuu, na matokeo ya Rais yahojiwe mahakamani.

Historia ya kuandikwa kwa Katiba Mpya ilianza Desemba mwaka 2011 wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akilihutubia taifa na baadaye aliwateua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba, ambayo ilianza kazi yake Mei 3, mwaka 2012.

Tume hiyo ilikusanya maoni ya wananchi nchi nzima na kuandaa Rasimu ya kwanza ya Katiba iliyotolewa Juni 4, 2013 kabla ya kutoa Rasimu ya pili ya katiba hiyo iliyoendelea kujadiliwa bungeni, huku wabunge wa upinzani wakisusia vikao hivyo ndipo lilipoibuka jina UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi), Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitakiwa kumaliza kazi ya kuandaa rasimu ya pili, lakini haikufanikiwa kukamilisha mpaka awamu ya Rais Kikwete ilipomalizika.

No comments :

Post a Comment