dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, July 26, 2018

Mzee Majuto kuanza kulipwa mamilioni ya fedha!

GOOD news! Msanii wa vichekesho Bongo, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ anatarajia kuanza kulipwa mamilioni ya fedha kutoka kwa watu walioingia naye mikataba isiyokuwa mizuri.

Akizungumza na Amani Jumatatu iliyopita, nyumbani kwake, maeneo ya Bunju jijini Dar, Majuto alisema aliamua kusamehe ile mikataba midogomidogo ila kwenye ile mikataba mikubwa aliyodhulumiwa ambayo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe aliahidi kumsaidia, ataendelea kusubiri kwani amepewa miezi miwili.

“Niliamua kusamehe ile mikataba yangu midogomidogo ila hiyo mingine aliyosema ataishughulikia muheshimiwa Mwakyembe bado naendelea kuisubiri ila kwa sasa siwezi nikaongea chochote kuhusu hilo, hivyo naomba mumuulize msemaji wa chama cha waigizaji,” alisema Majuto.

Amani pia lilifanikiwa kuongea na msemaji wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni, Masoud Kaftany ambaye alisema hatua aliyofikia Mwakyembe ya ufuatiliaji wa mikataba ya wasanii akiwemo mzee Majuto inaendelea vizuri na hivi karibuni kila kitu kitakuwa sawa. “Hivi karibuni alizungumza kwamba tutegemee baada ya miezi miwili au mitatu suala la mzee Majuto, Steven Kanumba pamoja na Wastara Juma litakuwa limeshamalizika hiyo mikataba,” alisema Kaftany.

No comments :

Post a Comment