dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 14, 2018

CCM imekununua kwa shilingi ngapi? Mtatiro atoa majibu haya!


CCM imekununua kwa shilingi ngapi? Ni miongoni mwa maswali ambayo Julius Mtatiro atakuwa akikutana nayo k wenye kila kona.

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya Uongozi CUF, amekutana na swali kama hilo kutoka kwa mtangazaji 2wa Azam TV, Charles Hilary.

Akijibu swali hilo Mtatiro amesema, "Sijui kama kuna mtu anaweza kuninunua kwa sababu nitakuchekesha kwamba viongozi wa chama cha Mapinduzi wakubwa akiwemo Katibu Muenezi wamekuja kunitafuta baada ya kushtuka nimezungumza na vyombo vya habari na watu hawakutarajia kama ninaweza kufanya mkutano na vyombo vya habari wa kuondoka."

"Kwa hiyo hata CCM wenyewe imekuwa surprise kwamba nimeomba kujiunga nao na jana na juzi ndio nilikuwa nafanya mawasiliano na chama changu kipya ambacho ninahitajika kuhamia na viongozi wanaendelea na maandalizi ili niweze kupewa utaratibu rasmi niweze kuchukua kadi, Kabla ya hapo sikuwa na mawasiliano na chama cha mapinduzi wenyewe," ameongeza.

Pia Mtatiro ameendelea kusisitiza kuwa kuondoka kwake ndani ya CUF na kuhamia CCM, alimuaga Maalim Seif na kutokana na ukomavu wake wa kisiasa wa kiongozi wake huyo hakuweza kuliweka wazi jambo hilo.

No comments :

Post a Comment