dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 27, 2018

Trump, Kenyatta kufanya mazungumzo leo White House!

Rais wa Marekani Donald Trump leo atakutana na mwenzake wa Kenya Uhuru Kenyatta katika ikulu ya White House, katika mkutano ambao unatarajiwa kuangazia zaidi masuala ya usalama na biashara.

Kenyatta anatarajiwa pia kutetea Kenya ipewe fursa zaidi ya kuuza bidhaa zake katika soko la Marekani, kando na kutafuta fedha za kufadhili miradi mikubwa ya miundo mbinu.Marekani inatarajiwa kutumia fursa hiyo kujaribu kupunguza ushawishi wa China ambayo imekuwa ikifadhili miradi mingi ya miundo mbinu Afrika miaka ya karibuni.

Kenyatta atakuwa rais wa tatu wa nchi ya Afrika kukutana na Bw Trump kwa mazungumzo ya kina nchini Marekani baada ya kukutana na Abdel Fattah Al Sisi Septemba mwaka jana na baadaye akakutana na Muhammadu Buhari wa Nigeria.

Asubuhi, Rais Kenyatta atakutana na wakuu wa kampuni mashuhuri nchini Marekani chini ya Baraza la Kibiashara la Uelewano wa Kimataifa kabla ya kwenda Ikulu ya White House kwa mashauriano na mwenyeji wake Rais Trump.

Kiongozi huyo wa Kenya anatarajiwa kukutana na Bw Trump katika afisi yake maarufu kama Oval Office katika ikulu ya White House kwa dakika 20.

Baadaye wawili hao wanatarajiwa kufululiza hadi kwenye Chumba cha Mikutano ya Mawaziri ambapo mazungumzo yatawashirikisha wajumbe waliosafiri na Bw Kenyatta na maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani.

Marekani ndiyo chanzo kikuu cha watalii wanaozuru Kenya na taifa hilo la Afrika Mashariki linatarajia kutumia fursa ya safari za moja kwa moja za ndege za Kenya Airways kati ya mataifa hayo mawili ambazo zitaanza Oktoba 28 kuimarisha idadi ya watalii wanaofika kenya.

Kibiashara, Kenya ni ya 85 kwa kuiuzia Marekani bidhaa duniani na wa jumla biashara kati ya mataifa hayo mawili huwa ya thamani ya jumla ya dola 1.5 bilioni za Marekani kwa mujibu wa Wizara ya Biashara ya Marekani.

Kenya inatafutaufadhili wa ujenzi wa barabara mpya kuu ya kutoka Mombasa hadi Nairobi, mradi unaotarajiwa kugharimu takriban dola 4.5 bilioni za Marekani.

Kenya hutazamwa kama mshirika muhimu wa Marekani katika vita dhidi ya ugaidi Afrika Mashariki na katika Upembe wa Afrika.

Mataifa yote mawili yana majeshi Somalia yakikabiliana na wapiganaji wa al-Shabaab.

No comments :

Post a Comment