dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 28, 2018

Trump, Kenyatta wakubaliana kujenga barabara kutoka Nairobi hadi Mombasa!



Marekani na Kenya zimekubaliana ujenzi wa barabara kubwa ya kutoka Nairobi hadi Mombasa. Makubaliano hayo yalikuja katika mazungumzo kati ya rais Donald Trump na Uhuru Kenyatta ambaye yuko ziarani mjini Washington.

Baada ya rais Trump kumkaribisha Kenyatta katika ofisi ya Oval kwenye Ikulu ya  White house , viongozi hao walielezea ushirikiano wa karibu wa kiuchumi, unaolenga kuyafanya mataifa hayo kuwa imara na ustawi wa wananchi wake. Mradi unaojulikana kama barabara ya Nairobi hadi Mombasa utaunganisha mji mkuu wa Kenya na ule wa pili Mombasa, na utajengwa na kampuni ya kimarekani ya Bechtel Corporation.


"Tumekuwa na uhusiano mzuri kabisa na Kenya, unakuwa mkubwa kila wakati . Tumo katika mpango mkubwa wa mradi wa miundombinu, barabara kubwa itakayoweka rekodi kwa njia tofauti na tutakamilisha mambo mengi mazuri", alisema Trump.

Mkurugenzi wa shirika la uwekezaji la Marekani alikutana mwezi uliopita na kampuni ya ujenzi ya Bechtel nchini Kenya kuhusu utayari wa shirika hilo juu ya mradi, unaochukuliwa na Marekani kama njia ya kushindana na uzinduzi wa mipango ya China ya ujenzi wa barabara na reli barani afrika na mahali pengine. Mwaka jana Kenya ilifungua njia ya reli iliyofadhiliwa na China kati ya Nairobi na Mombasa, ambayo inaelezwa na Kenya kuwa mradi mkubwa wa miundombinu tangu uhuru.

Taarifa ya Ikulu ya White House imesema pande zote zimekubaliana kutafuta ushauri zaidi ili kukamilisha masharti ya makubaliano ya ufadhili. Viongozi hao wawili pia walitangaza kwamba serikali zao zimeanzisha safari za moja kwa moja za ndege kati ya Nairobi na New York.

"Tumekuwa na ushirikiano bora, hususan katika mapambano yetu dhidi ya ugaidi kwasababu ya ujirani tulioko, tuko katika mapambano na Al-shabaab, ambayo Marekani imekuwa mshirika muhimu na imara. Muhimu zaidi tuko hapa kwa ajili ya kutafuta na kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji, ambao tayari uko imara", Kenyatta aliwaeleza waandishi wa habari.

White House imeongeza kwamba "mikataba mingine ya kibiashara inayogharimu karibu dola milioni 900 iliyotangazwa wakati wa ziara hiyi itaweza kutengeneza ajira nyingi baina ya Wamarekani na Wakenya, na baadae kuwezesha ustawi na ushindani wa kiuchumi wa mataifa yote mawili". Trump amekuwa akikosolewa kwa kutozipa kipaumbele nchi za kiafrika na kutakiwa kuomba msamaha mapema mwaka huu, baada ya maoni yake binafsi aliyosema nchi za kiafrika na nyingine zina uozo, kuvuja kwa waandishi wa habari.

No comments :

Post a Comment