airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, September 3, 2018

Amana benki na taasisi kutoka Kuwait kuanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu!

Amana Bank kwa kushirikiana na Taasisi ya Direct Aid ya Kuwait imeamua kuunga mkono juhudi za serikali na malengo ya Taifa ya sekta ya Elimu kwa kuwasaidia wanafunzi wa vyuo vikuu hapa ' nchini ambapo wanafunzi 500 watakaokosa mikopo watasoma bure kila mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye utiaji saini Mkurugenzi wa Amana benki Dkt. Mohsin Masood amesema kuwa kwa kuanzia taasisi hizi zitasaidia kutoa mikopo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Morogoro kwa Tanzania Bara na Chuo cha Sumait kwa upande wa Zanzibar.

"Taasisi hizi zitatoa mikopo isiyo na riba kwa wanafunzi wa vyuo hivi hususan wale ambao hali yao ya kiuchumi ni duni na hawajapata mikopo kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB)" amesema  Dkt. Masood.

Makubaliano hayo yaliyofikiwa na taasisi hizo yamesainiwa leo na Mkurugenzi mtendaji wa Amana Bank. Dr. Muhsin Salim Masoud na Dr. Abdulrahman Al muhailan  kwa upande wa Direct Aid katika ukumbi wa Serena HoteI.

Aidha lengo kuu la kusaini makubaiiano haya ni kutimiza azma ya kuwawezesha wanafunzi kupata elimu ya juu ili kuongeza nguvu kazi ya Taifa hasa katika kipindi hiki muhimu cha kujenga Uchumi wa Viwanda.

Amana Benki imedhamiria kuitizama sekta ya elimu kipekee ikiwa ni kutambua umuhimu wa Elimu katika maendeleo ya Taifa letu. Dhamira hii imeisukuma Amana Bank kuwa mtari wa mbele katika kutengeneza na kutoa huduma mbali mbali zinazohusiana na kuboresha sekta hii ikiwemo akaunti ya mwanafunzi na akaunti ya watoto ambazo husaidia wazazi. walezi na watoto kuweka akiba kwa ajili ya kutimiza ndoto ya kupata elimu bora.

Mbali na huduma hizi na makubaliano haya yakutoa mikopo. Amana Bank pia ipo katika hatua z mwisho za mazungumzo na vyuo vikuu na taasisi nyengine za Elimu nchini katika kuangalia namna bora ya kutoa mikopo kwa wanafunzi itakayoendana na kunyanyua udahili kwa taasisi hizo na kuboresha miundo mbinu na vitendea kazi kwa ajili ya kufanikisha utoaji wa huduma ya Elimu kupitia huduma mpya ya Elimu itakayozinduliwa hivi punde.

Ukuaji huu unaenda sambamba na upanuzi wa huduma kuyafikia makundi mbalimbali ya wananchl hasa wale wa kipato cha chini. Kwa muda usiozidi miaka miwili toka Amana Bank ilipoanza kuwawezesha wafanyabiashara wadogo imefanikiwa kuwawezesha jumla ya kiasi cha zaidi ya fedha za kitanzania Bilioni 6.2 (Site nukta mbili).

Katika kuongeza kasi ya ujumuishajl wa huduma za kifedha kwa watanzania wa kipato cha chini. Amana Benki inatarajia hivi punde kuanza kutoa uwezeshaji kwa vikundi vya wafanyabiashara

wadogo wadogo (Solidarity Group Financing SGF) ambapo uwezeshaji huu utanza kutolewa.

No comments :

Post a Comment