dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, September 26, 2018

Donald Trump aijia juu Iran!

Rais Donald Trump wa Marekani

Mshauri wa Taifa la Marekani wa masuala ya Usalama wa rais Donald Trump,John Bolton, amewaonya watawala wa Iran kwamba kutakuwa na - akitamka kwa maneno yake, jehanamu ya malipo, endapo watajaribu kuishambulia Marekani, raia wake, ama washirika wake.Rais Trump ameyasema hayo katika mkutano wa kutoiunga mkono Iran mjini New York amesema katika kile alichokiita ''utawala wa mauaji'' wa "mullah kutoka Teheran" utakabiliana na matokeo mabaya endapo wataendelea 'kusema uongo, kudanganya, na kudanganya'.

Bolton amenukuliwa akisema kuwa Marekani itakuwa kali katika kutekeleza vikwazo vya kiuchumi kwa Iran ambavyo vinaanza baada ya Marekani kujitoa katika mpango wa nyuklia wa mwaka 2015.

Alisema kuwa Umoja wa Ulaya au mtu mwingine yeyote hataruhusiwa kuwadhoofisha. Mapema waziri wa mambo ya nje nchini Marekani, Mike Pompeo, aliushutumu kwa nguvu zote Umoja wa Ulaya kwa kuanzisha utaratibu maalum wa kulipia vikwazo vya mafuta.Pompeo amedai kwamba kuendeleza mapato kwa Teheran ingeweza kuimarisha msimamo na nafasi ya Iran kama mfadhili wa serikali ya ugaidi.

No comments :

Post a Comment