dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, September 12, 2018

Mbunge CUF Apigilia Msumari Sakata la Makontena ya Makonda!

Mbunge wa Konde, Khatibu Saidi Haji (CUF), amemsifu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango kwa ‘kuyang’ang’ania’ makontena ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akimtaka kuyalipia kodi.

Makontena hayo ambayo yaliingizwa Bandari ya Dar es Salaam kwa jina la mkuu huyo wa mkoa yakidaiwa kuwa na samani za walimu wa shule mbalimbali za Mkoa wa Dar es Salaam ambapo yalitakiwa kulipiwa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), yakitakiwa kulipiwa kodi suala lilioungwa mkono na Waziri Mpango na kuamuru yazuiliwe hadi yatakapolipiwa kodi na yasipolipiwa yapigwe mnada huku Rais John Magufuli akipigilia msumari wa mwisho kumtaka Makonda ayalipie kodi makontena hayo.Akichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia Baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), bungeni jijini Dodoma leo Jumatano Septemba 12, Haji amesema mawaziri wa aina ya Dk. Mpango ndiyo Rais Magufuli anaowataka.

“Mheshimiwa sheria ni msumeno na katika kutekeleza majukumu yako muhimu ya kusimamia fedha za nchi hii hutakiwi kumwangalia usoni yeyote anayevunja sheria za nchi hii katika kusimamia kodi za wananchi.

“Kwa hiyo kitendo chako kitabakia katika historia, alijaribu kuwachezea wengine lakini alichezea vyeupe amekutana na cheusi kimemtia doa, na nakuambia Dk. Mpangio uzi ni huo huo mbane Makonda hadi mwisho ili haki ipatikane,” amesema Khatibu.

No comments :

Post a Comment