dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 2, 2018

Treni bora duniani yawasili nchini ikiwa na watalii 64!

TRENI ya kifahari inayojulikana kwa jina la ROVOS ambayo ni miongoni mwa treni tatu bora duniani imewasili jijini Dar es Salaam kwa kutumia reli ya Tazara ikiwa na watalii 64.

Watalii hao wamekuja Tanzania kwa ajili ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye vivutio vya utalii hapa nchini ikiwemo mbuga za wanyama na visiwa vya Zanzibar.

Akizungumza katika hafla fupi ya kuwapokea watalii hao iliyofanyika stesheni ya TAZARA Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa TAZARA Tanzania, Fuad Abdallah alieleza kuwa treni hiyo iliondoka mji wa Cape Town nchini Afrika ya Kusini Agosti 18, mwaka huu.“Watalii mbalimbali huja nchini mara tano kwa mwaka kwa kutumia ROVOS kupitia reli ya TAZARA na nchi yetu hunufaika na ujio huu hasa faida za kiuchumi,” alisema Fuad. Aidha alibainisha kuwa treni ya ROVOS ni miongoni mwa treni tatu bora duniani, hivyo ujio wa treni hiyo na watalii unatokana na vivutio bora vya utalii na miundombinu mizuri ya reli ya TAZARA. “Treni hii inatumia reli ya TAZARA kuleta watalii kwa sababu nchi yetu imekidhi vigezo vya utalii na reli yetu imekidhi vigezo vya usalama na mawasiliano ya uhakika,” aliongeza Fuad.

Alisema kuwa katika safari hiyo ya treni watalii hao pia walipata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Selous iliyopo kusini mwa Tanzania na kuona wanyama mbalimbali wanaopatikana kwenye hifadhi hiyo.
Wakizungumza kwa furaha ya kuwasili Tanzania, watalii hao wa kijerumani walisema kuwa wamefurahia sana safari hiyo na mapokezi mazuri ya watanzania na kuahidi kurudi kwa mara nyingine.

Kwa upande wake mfanyakazi wa treni ya ROVOS, Monica Rieder mwenye asili ya Ujerumani alisema kuwa amewahi kufika Tanzania mara 14 na anavutiwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo yanayofanyika hapa nchini siku hadi siku. TAZARA ni shirika la reli ya pamoja ya Tanzania na Zambia iliyoanza mwaka 1976 na inamilikiwa kwa asilimia 50 kila upande.

No comments :

Post a Comment