dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 23, 2018

Wajumbe wa baraza la wawakilishi wapewa semina!


Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi,Atashasta Nditie amewataka wajumbe wa baraza la wawakilishi kuweza kupitia ,kuijadili pamoja na kutoa michango yao katika Rasimu ya kanuni ya namna ya uendeshaji wa miundo mbinu ya kimkakati ambayo imetungwa chini ya shirika la mawasiliano kwa maslahi mapana ya taifa.

Hayo Ameyaeleza wakati akifungua kikao cha siku moja cha kujadili pendekezo la kutunga kanuni za shirika la mawasiliano Tanzania, TTCL 2018, Kutoa maoni kuhusu itifaki ya jumuiya ya afrika mashariki kuhusiana na masuala ya tehema na mapendekezo ya kufanyia marejeo sera posta ya mwaka 2003.Naibu waziri Alisema wizara ya mawasiliano Tanzania imekuja na mkakati uliobora wa kuimarisha sekta ya mawasiliano ambapo kwa sasa wapo katika hatua ya kukusanya maoni toka pande zote za muungano ili kuhakikisha sheria ya kuanzisha shirika la mawasiliano Tanzania inakamilika huku ikiwa na maoni kwa wadau toka sehemu zote za muungano.

“napenda kuchukua fursa hii kuwaomba wajumbe wa baraza tuchangie maeneo yoyote ambayo mnaona yanahitaji kutungiwa kanuni ambazo zitawezesha dhamira ya serikali kuwa na shirika ambalo linachangia uchumi wa nchi” alisema Mhandisi Nditie.

Alisema lengo la kikao kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi ni kuwakutanisha na wataalamu kutoka Tanzania bara ili kuweza kuandaa nyaraka ambazo zina maoni Kutoka tanzania bara na tanzania visiwani.

Aidha alisema kukamilika kwa rasimu hiyo kutawawezesha watanzania kwa ujumla kuweza kunufaika kutokana ubora wa huduma za mawasialino kutoka katika shirika la mawasiliano Tanzania.

Hata hivyo alisema Hata hivyo Alisema kutokana na kukua kwa kwa teknolojia ya mawasiliano na maendeleo katika sekta ya posta imelazimika kufanya marejeo ya sera ili kuweza kuendana na kasi ya maendeleo na shirika ambalo linachangia kukua kwa uchumi wa nchi.
Nae mwenyekiti wa kamati ya mawasiliano baraza la wawakilishi mhe, Hamza Hassani Juma alisema Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya mawasiliano ya baraza la wawakilishi Hamza Hassan Juma amesema watahakikisha wanachangia vyema ili kuona kunaongezeka tija ya utekelezaji wa majukumu wa shirika la mawasiliano.

Aidha alisema anashukuru kuona maoni ambayo wameshauri kama kamati ya mawasiliano juu ya mambo ya muungano kuweza kushirikishwa juu ya mambo yote yenye maslahi na taifa.

Kwa upande wake Naibu waziri wa Mawasiliano na uchukuzi Zanzibar alisema hatua iliyofikiwa na wizara ya ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Tanzania imekuja kuondoa moja ya kero ya muungano ambapo pande zote mbili zinaposhirikishwa katika kutoa maoni juu na sheria yoyote na masuala muhimu yenye maslahi kwa taifa.

“Kuna sheria nyingi za muungano zilikuwa zinapitishwa bungeni huku zanzibar ikiwa inasikia tu bila ya kushirikishwa hivyo kwa sasa ni hatua muhimu sanaa imefikiwa na wizara hii ili kuondoa kero na manung’uniko toka pande yoyote ya muungno”

Kikao hicho cha siku moja kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi kilifanyika katika ukumbi wa baraza hilo uliopo chukwani nje kidogo ya mji wa zanzibar.

No comments :

Post a Comment