Meghan Markle, mkewe Mwanamfalme wa Harry nchini Uingereza ni mja mzito na anatarajiwa kujifungua mwaka ujao wa machipuko, kasri la Kensington limefichuwa.
Tangazo hilo linajiri wakati Meghan, mwenye umri wa miaka 37, na mwanamfalme Harry, mwenye miaka 34, waliofunga ndoa huko Windsor miezi mitano iliyopita, waliwasili Sydney Jumatatu katika kuanza kwa ziara ya siku 16 nchini Australia na New Zealand.
Kasri la Kensington limesema wanandoa hao wana "furaha kutangaza habari hii njema kwa umma".Mtoto wao atakuwa wa saba katika orodha ya ufalme.
Malkia na maafisa wengine wa ufalme waliambiwa kuhusu habari hizo njema siku ya Ijumaa, wakati familia ya kifalme ilipokusanyika Windsor kwa harusi ya mwanamfalme Eugenie.
Meghan alihudhuria harusi na mumewe Harry, akionekana kuvaa, koti refu la samawati, hatua iliyozusha minong'ono kwamba huenda ni mja mzito.
Fununu hizo zilizidi alipoonekana kujiziba kwa bahasha mbili kubwa tumboni alipowasili Sydney, katika ziara yao rasmi ya kwanza tangu walipooana, ambayo ilifanyika katika kanisa la St George's huko Windsor.
Wataanza shughuli Jumanne ambapo umma unatarajiwa kuwatakia heri na kuwapongeza.
Wanandoa hao wanaofuata nyayo za wazazi wa Harry - Mwanamfalme Charles na Diana, Mwanamfalme wa Wales - ambayo ziara yao ya kwanza ilikuwa ni Australia na New Zealand.
Harry na Meghan hawakuficha azma yao ya kupata watoto.
Katika mahojiano mnamo 2016 Meghan alisema, kuwa mama ni jambo 'analolitazamia' , na Harry katika mahojiano yao walipochumbiana alisema: "Unajua , nafkiri kila hata na wakati wake, na pengine tutakuwa na familia katika siku za hivi karibuni."
Mtoto wao atakuwa bin amu wa Wanamfalme George, Charlotte na Louis - lakini hatokuwa mwanamfalme hadi iwapo Malkia ataingilia kati kabla ya kuzaliwa.
Harry na Meghan walikutanishwa kwa siri na rafiki wao pamoja na walichumbiana miezi 16 baadaye.
Meghan alipata umaarufu kwanza kutokana na uigizaji, katika filamu ya kuigiza Marekani - Suits, lakini aliachana na kuigiza alipoolewa.
Watu tofuati duniani wamewapongeza wanandoa hao.

No comments :
Post a Comment