dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, November 19, 2018

Kangi Lugola aibukia Zanzibar!

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameibuka visiwani Zanzibar kwa ajili ya ziara ya Kikazi visiwani humo ambapo amekutana na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Rais wa Zanzibar Dkt Ally Mohamed Shein.

Waziri huyo amekutana na Rais wa Zanzibar Dkt Shein leo novemba 19 ikulu ambapo alifika ofisini kwa kiongozi huyoo wa nchi kwa nia ya kujitambulisha akiambatana na baadhi ya viongozi wake wa wizara.

Miongoni mwa viongozi walioambatana na Kangi Lugola ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Kailima Ramadhani.Hii ni mara ya kwanza kwa Kangi Lugola kuwasili visiwani humo tangu alipoteuliwa na Rais Magufuli kushika nafasi hiyo julai 1 mwaka huu baada kuenguliwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kushindwa kudhibiti ajali za barabarani.

Vilevile katika siku za hivi karibuni Visiwani Zanzibar kulisambaa taarifa za Jeshi la Polisi kuwakamata wanaume 10 ambao walitajwa kujihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.

No comments :

Post a Comment