dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, February 18, 2019

Anasa Uwanja wa ndege kwa miezi mitatu!


Raia mmoja wa Niger ambaye amefurushwa nchini Israeli amenasa uwanja wa ndege nchini Ethiopia toka mwezi Novemba mwaka jana.

Eissa Muhammad, 24, amenasa kwenye kiwanja hicho jijini Addis Ababa baada ya nchi yake kugoma kumpokea.

"Nimekuwa nikikaa hapa (uwanja wa ndege) katika mazingira magumu, hakuna kitu, hakuna kitu kabisa..." Muhamad ameiambia BBC.

Mikasa ilianza kumuandama Muhamad mwezi Aprili mwaka jana baada ya kunaswa akiishi Israeli bila ya kibali, Kijana huyo alihamia Israeli kutoka Niger mwaka 2011, akiwa na miaka 16 ili kutafuta maisha bora.

Anasema aliwalipa wasafirishaji wa binaadamu ili kumpitisha nchini Libya na Misri kabla ya kuingia Israeli kwa miguu, Alipofika jijini Tel Aviv, Tel Aviv, Muhamad aliishi kwa kutegemea kazi duni kwenye majumba ya kuishi wanafunzi na kiwanda cha kuzalisha pipi.

Baada ya kushikiliwa kizuizini kwa zaidi ya miezi sita, Israeli ilimpatia hati ya dharura ya kusafiri na kumpakia kwenye ndege ya Shirika la Ethiopia kuelekea Niger kupitia Addis Ababa mwezi Novemba.

No comments :

Post a Comment