dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, February 22, 2019

ZANZIBAR STARTS RATIONING ELECTRICITY!


ZECO yatangaza mg ao wa umeme kisiwani unguja kuanzia Ijumaa February22,2019.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la umeme Zanzibar ZECO imesema lipokwenye mpango wa kutafuta mbinu mbadala Ya kupata umeme wa ziada ili kupunguza usumbufu kwa wananchi pindi umeme mkubwa wa Tanesco ukikatika kutoka Tanzania bara.


Akizungumza na Waandishi wa habari Afisa Uhusiano kutoka kwenye shirika hilo Salum Abdalla Mohamed amesema shirika la umeme tanesco hivi sasa litazima umeme na kuanza kutoa kwa mgao bara na visiwani kutokana na kufanya matengenezo kwenye eneo la Ubungo.

Amesema kuwa kuanzia leo Ijumaa wananchi wanakuwa wanazimiwa umeme na kupata kwa mgao na hali hiyo itaendelea hadi juni mwezi wa sita kutakapokamilika matengenezo kwenye eneo linalotengenezwa.

Aidha salum amewataka wananchi hususani wafanyabiashara wanaotumia umeme kwa kiwango kikubwa kuwa wavumilivu kwani shirika hilo wanatengeneza ili kuleta maendeleo nchini.

Amesema serikali inatambua kuwa umeme ni nishati muhimu sana kwa wananchi nandio maana inafanya kila jitihada kuhakikisha wananchi wanapata huduma hiyo bila usumbufu.

Salumu amesema mgao huo utakuwa kwa Unguja kwani ndio wanaotegemea umeme kutoka Tanzania bara ila Pemba hawatohusika kwani wao umeme wanapata kutoka tanga.

Hivi karibuni Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Dk John Pombe Magufuli aliliagiza Shirika la Tanesco kufuta deni la umeme wanalodaiwa shirika la umeme Zanzibar ZECO.

No comments :

Post a Comment