dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, April 21, 2019

Watu 137 wapoteza maisha baada ya makanisa na hoteli kushambuliwa!

Watu 137 wameuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa katika msururu wa mashambulio dhidi ya makanisa na hoteli Sri Lanka, vianzo vya polisi na hospitali vimesema.

Milipuko sita imeripotiwa katika mashambulio dhidi ya makanisa matatu mjini Kochchikade, Negombo na Batticaloa ambayo yalisahambuliwa wakati wa ibada ya Pasaka.

Hoteli za The Shangri La, Cinnamon Grand na Kingsbury ambazo zipo mjini Colombo, pia zililengwa katika mashambulia hayo.

Jumapili ya Pasaka ni moja ya siku kuu muhimu sana katika kalenda ya waumini wa dini ya Kikristo.

Hakuna kundi lolote lililojihusisha na mashambulizi hayo.

Kumekua na hofu huenda wapiganaji wa kundi la Islamic State waliorejea kutoka mashariki ya kati wakawa tishio kwa usalama wa nchi hiyo.

Kanisa la St Sebastian mjini Negombo lilmeharibiwa vibaya na milipuko hiyo.

Picha zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha paa la jengo la kanisa lililoharibiwa vibaya huku damu ikiwa imetapakaa ndani ya kanisa.

Karibu wati 67 wameripotiwa kufariki ndani ya kanisa hilo.

Pia kumeripotiwa idadi kubwa ya watu waliyojeruhiwa katika kanisa la St Anthony mjini Kochchikade, ambao ni moja ya wilaya ya Colombo.

Raia tisa wa mataifa ya kigeni ni miongoni mwa watu waliouawa mjini Colombo, kwa mujibu wa vianzo vya hospitali vilivyozungumza na BBC.

Vyanzo sawia na hivyo mjini Batticaloa vimesema kuwa karibu watu 27 wamefariki mjini humo.

Afisa wa hoteli ya Cinnamon Grand, karibu na makao rasmi ya waziri mkuu wa nchi hiyo,ameiambia shirika la habari la AFP kuwa mtu mmoja alifariki kutokana na mlipuko huo.

Rais Maithripala Sirisena ametoa tarifa ya kuwaomba wananchi kuwa watulivu na kuwasaidia maafisa wake katikan uchunguzi.

Waziri mkuu Ranil Wickremesinghe ambaye anaongoza mkutano wa dharura. Amesema: "Nalaani vikali shambuliowatu wetu leo. Natoa wito kwa Wa Sri Lanka wote kuungana wakati huu mgumu."

Katika mtandao wake wa Twitter, Waziri wa Fedha Mangala Samaraweera aliandika mashambulio haya yamepangwa na kutekelezwa ili "Kuua watu, kusababisha taharuki na kugonganisha watuw" na yamesababisha vifo vya "watu wengi wasiokua na hatia".

Waziri mwingine , Harsha de Silva, amesema mashambulio hayo ni ya kuogofa "Nimeona hali ya kusikitisha " katika kanisa la St Anthony Shrine mjini Kochchikade, ana kuongeza kuwa ameona " vipande vya miili ya watu iliyotapakaa kila sehemu".

No comments :

Post a Comment