dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 23, 2019

Korea Kaskazini haina mpango wa kujadili kuhusu nyuklia!

Korea Kaskazini imesema leo kuwa haina shauku katika majadiliano hadi pale Marekani itakapoacha kuongeza hatua zake za uhasama, wakati mjumbe mwandamizi wa Marekani akifanya ziara nchini Korea Kusini akilenga katika kufufua mazungumzo ya kinyuklia na Korea kaskazini.

Mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Marekani yamekwama tangu mkutano wa pili kati ya rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un katika mji mkuu wa Vietnam, Hanoi mwezi Februari kuvunjika bila makubaliano.
Viongozi hao wawili walikutana mwezi Juni katika eneo lililotengwa bila shughuli za kijeshi kati ya Korea mbili na kukubaliana kuanzisha tena majadiliano katika ngazi ya mashauriano, lakini mazungumzo hayo bado hayajaanza.

Wakati huo huo Korea Kaskazini imefanya majaribio kadhaa ya makombora ya masafa ya kati ikipinga luteka ya pamoja ya kijeshi ya kila mwaka kati ya Marekani na Korea Kusini.

No comments :

Post a Comment